Jamii

Athari za Nyota katika Kazi Unazofanya-Je Kazi ipi Inakufaa?

athari-za-nyota-katika-kazi-01

Unajimu unaeleza uhusiano uliopo kati ya alama 12 za nyota katika anga na tabia mbalimbali za binadamau na mambo mengine katika maisha yao duniani. Tabia hizi tofauti za binadamu zinachangia kwa namna moja au nyingine watu tofauti kufanya vizuri katika kazi moja na si nyingine,athari za nyota katika kazi wanazofanya zinaelezwa kuwa wazi katika unajimu.

Kama nyota yako inachangia wewe kuwa mpole na mwenye huruma basi utafaa zaidi ukiwa nesi au mfanyakazi katika misaada kwa watu kuliko kuwa askari. Hapa tutaonyesha tabia watu katika nyota 12 na kazi zinazoendana na wasifu wao ambazo zitawawezesha kufanikiwa zaidi katika wanachokifanya.

Soma pia:

Nyota ya Kondoo (Aries): Machi 21 – Aprili 19

athari-za-nyota-katika-kazi-ujenzi
Tabia:
Watu wenye nyota hii ni chakalamu na watendaji na wanaojiamini. Wanaongozwa na sayari ya Mars. Ni watu wenye kutaka uwazi na ukweli. Wanafanya mabo kwa haraka na hawana uvumilivu wa kusubiria.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • zinazohusisha serikali
 • ujenzi
 • elimu

Nyota ya Ng’ombe (Taurus): Aprili 20 – Mei 21

athari-za-nyota-katika-kazi-uhasibu
Tabia:
Ni watu wenye kuaminika na ni watekelezaji kwa vitendo zaidi. Wanachukua maamuzi kutokana na vigezo na vigezo na sio hisia pekee. Wanaongozwa na sayari ya Venus ambayo huwafanya wapende starehe na vitu vya thamani.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • zinazohusiana na fedha,
 • utunzaji wa mahesabu ya fedha au uhasibu na
 • Pia wanaweza wakawa wasanii wazuri wa urembeshaji na mapambo.

Nyota ya Mapacha:(Gemini ): Mei 22 – Juni 20

athari-za-nyota-katika-kazi-uchoraji
Tabia:
Ni watu wenye kutaka vitu tofauti kila mara na wanachoshwa sana na mazingira na mitindo ileile isiyobadilika. Wanaomngozwa na sayari ya zebaki. Wanapenda kuongea na kuwasiliana.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • uchoraji ramani za majengo,
 • ubunifu na
 • Kwasababu ni wawasiliani wazuri wanafaa pia kufanya kazi za masoko.

Nyota ya Kaa(Cancer): Juni 21 – Julai 22

athari-za-nyota-katika-kazi-unesi
Tabia:
Ni watu wenye hisia kali,moyo mzuri na wenye ndoto. Wanaongozwa na Mwezi. Ni watu wenye kutetea wengine na wanaopenda kuwa katika mazingira waliyoyazoea.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • Unesi
 • Huduma za sheria na haki
 • Masula ya saikolojia
 • Masuala za historia

Nyota ya Simba(Leo): Julai 23 – Agosti 22

athari-za-nyota-katika-kazi-burudani
Tabia:
Ni watu wenye asili ya uongozi, wenye mvuto wa kupendwa na wenye matarajio na matumaini katika kazi zao. Wanajiona na wanapenda madaraka na nguvu.
Wanaongozwa na jua,wanahitaji sana kuwa mbele na kuonekana.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • Kutoa burudani
 • Uhandisi na ujenzi wa majumba

Nyota ya Mashuke(Virgo):Agosti 23 – Sept 22

athari-za-nyota-katika-kazi-utafiti
Tabia:
Ni watu wenye kupenda kufuatilia na kujua mambo kwa undani, na wanapenda kujifunza na kujua maana ya kila wanachokifanya.
Wanaonzozwa na sayari ya Zebaki.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • Masula yanayohusu jamii
 • Uandishi na uhariri
 • Masuala yanayohitaji Utafiti na uchambuzi

Nyota ya Mizani (Libra): Sept 23 – Okt 22

athari-za-nyota-katika-kazi-sheria
Tabia:
Ni watu wenye asili ya kidiplomasia na wenye kupendwa na watu.
Wanaongozwa na sayari ya venus. Ni watu wenye kushirikiana kwa asili. Wanapenda haki na usawa.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • Masula ya sheria
 • Muziki
 • Sanaa
 • Uigizaji

Nyota ya Ng’e (Scorpio): Okt 24- Nov 21

athari-za-nyota-katika-kazi-uchambuzi
Tabia:
Ni watu wenye asili ya uchambuzi na upelelezi,wana uwezo mkubwa wa kupembua mambo na ni wenye ufahamu mkubwa. Wanaongozwa na sayari ya Mars. Wanauwezo wa kuchimba ndani ya akili ya mtu na kuona siri zote.
Ni watu wasiowazi juu ya hisia zao.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • Upelelezi na uchambuzi
 • mambo ya sheria
 • Siasa

Nyota ya Mshale (Sagittarius): Nov 22- Des 21

athari-za-nyota-katika-kazi-masoko
Tabia:
Ni watu wenye mawazo ya matumaini mazuri na maadili mazuri.
Wanapenda masuala ya kiroho na kusafiri. Wanaongozwa na sayari ya jupita.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • Mahusiano ya kijamii
 • masoko
 • Teknolojia ya habari na mawasiliano
 • Utalii

Nyota ya Mbuzi(Capricorn):Des 22 – Jan 19

athari-za-nyota-katika-kazi-tehama
Tabia:
Ni watu wasiokata tamaa na wenye kubeba majukumu yao vizuri. Wanapenda kufanya mambo yenye njia zilizo wazi na kufuata taratibu na zenye uhakika.
Wanaongozwa na sayari ya Satani. Ni watu wenye adabu ya hali ya juu katika mambo wanayoyafanya na wenye malengo thabiti.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • Mambo yanayohusu Sayansi
 • Uongozi
 • Teknolojia ya habari na mawasiliano

Nyota ya Ndoo (Aquarius):Jan 20 – Feb 18

athari-za-nyota-katika-kazi-sayansi
Tabia:
Ni watu wenye kupenda uhuru na kujitegemea. Ni wabunifu na watafiti wa mambo. Ni watu wasio wa kawaida. Wanaongozwa na sayari ya Satani.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • Mambo yanayohusu Sayansi
 • Teknolojia
 • Sayanzi ya Komputa

Nyota ya Samaki (Pisces):Feb 19 – Machi 20

athari-za-nyota-katika-kazi-jamii
Tabia:
Ni watu wenye kupenda na kujali wengine. Hawana ubinafsi na ni wenye mapenzi makubwa katika uhusiano.
Wanaongozwa na syari ya Jupita.

Kazi:
Kazi zinazowafaa ni:

 • Mambo yanayohusu jamii
 • Mambo ya afya
 • Uongozi

Je kuna madhara yoyote ya nyota katika kazi  yako?

Kama kuna athari za nyota katika kazi kwa upande mwingine inabaki kuwa imani zaidi, kuna wasioamini kuwa kuna madhara yoyote ya nyota kama wanajimu wanavyosema. Lakini wewe unaonaje? Tabia hizi zinaendana na za kwako kulingana na tarehe uliyozaliwa? Kama ndiyo basi unajimu ni sayansi na unaweza kutumika kukuongoza katika kufanya kazi sahihi itakayokuletea mafanikio.
Tupe maoni na mtazamo wako juu ya mada hii na elimu ya unajimu. Andika katika sanduku la majibu hapo chini na ushiri

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment