Afya Zetu

Homa ya Dengue: Dalili zake na Jinsi ya Kujikinga

aedes_aegypti

Dengue (hutamkwa DENGU) ni homa yenye maumivu makali, yanayosababishwa na kuumwa na mbu mwenye kusambaza virusi vya dengue. Virusi hivi vinahusiana na virusi vinavyosababisha homa ya manjano.

Dengueinasambazwa na mbu aina ya Aedes hasa hasa kabila la A.aegypti.

Mbu hawa huuma wakati wa mchana tofauti na wale wa malaria ambao huuma usiku.

Homa ya dengue inasambaa kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes wenye maambukizo virusi vya dengue. Dengue haiwezi kuenea moja kwa moja kutoka kwa mtu mmoja hadi mtu mwingine.

Dalili za homa ya dengue
Dalili, ambayo kwa kawaida huanza siku 4-6 baada ya kuambukizwa na hadi kufikia siku hadi 10, ni pamoja na:

 • homa ya ghafla
 • maumivu makali ya kichwa
 • Maumivu nyuma ya macho
 • Maumivu ya misuli
 • Kichefuchefu
 • Kutapika
 • Upele kwenye ngozi, ambayo huonekana siku tatu hadi nne baada ya maambukizo
  Kutokwa na damu (kama puani , fizi n.k)

Dalili hizi zinaweza kuwa sawa na baadhi ya magonjwa mengine hasa malaria

Watoto wadogo na watu ambao hawajawahi kupata maambukizi haya kabla huathirika zaidi kuliko watoto wakubwa na watu wazima.

aedes_aegypti_feeding

Mbu aina ya Aedes Aegypti akiwa anauma mwili wa binadamu

Kinga ya Mambukizo ya Dengue
Hakunachanjo iliyopitishwa kwa ajili yavirusi wa dengue. Hivyo njia pekee ni kujilinda dhidi ya mbu wenye maambukizi ya dengue.

Baadhi ya hatua za kuchukua ni kama ifuatvyo:

 1. Kunyunyizia dawa ya kufukuza na kuua mbu ndani ya makazi ya watu
 2. Kunyunyiza au kupaka dawa ya kufukuza mbu mwilini
 3. Kuvaanguo ndefu zisizobana ili kuzuia mwili
 4. Kulalandani yachandaruaili kuepukakuumwawakati wa usiku na mchana pia
 5. Kuweka mazingira katika usafi ili kuzuia mbu kuzaliana na kupumzika. Hakikisha madimbi ya maji karibu na makazi yanafukiwa au kunyunyiziwa dawa ya kuua wadudu pamoja na mbu.

Kama unahisi dalili za homa na uchovu kama ilivyoelezwa hapo juu tafadhari wahi hospitali kwa msaada zaidi.

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment