Michezo

Huzuni….. Mzee Small wa Bongo Movie Afariki Dunia!!

Small-Mzee

Muigizaji gwiji hapa nchini Said Wangamba”Mzee small” amefariki dunia usiku wa wa kuamkia leo katika hospitali ya taifa muhimbili alipokuwa akifanyiwa matibabu.

Taarifa ya kifo cha mzee small zimethibitishwa na mwanae anayeitwa Mahmoud Wangamba, aidha Mahmoud alisema baba yake amefariki usiku wa jana katika hospitali ya taifa muhimbili alipokuwa akifanyiwa matibabu yake.

Mipango ya msiba inafanyika nyumbani kwao Tabata , hizi ni taarifa za awali kwa taarifa zaidi tutaendelea kukuhabarisha kila habari zinapotufikia.

Kifo cha gwiji huyo wa filamu kimeongeza simanzi katika tasnia ya filamu na taifa kwa ujumla baada ya majuma kadhaa kuwapoteza watu muhimu katika tasnia hiyo pia.

Bongoposts pamoja na uongozi wake unatoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na watu wote walioguswa na msiba huo.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi amen.

&nbsp

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment