Fedha na Uchumi Mafanikio

Je unataka Kuwa Tajiri?,Anza Kufikiri kama Matajiri

Namna ya Kuwa Tajiri

Masikini na matajiri wanatofautiana sana kwa jinsi ambavyo wanafikiri. Imefahamika kuwa matajiri wote wanafikiri kwa namna inayofanana wakati masikini wanafikiri tofauti sana nao. Ukitaka kuwa tajiri ni muhimu kufahamu juu ya tofauti hizi za kifikra.

Siri hii peke yake inachangia kwa kiasi kikubwa utofauti wa makundi haya mawili ya watu-matajiri na masikini.

Badiri Fikra:

ukitaka Kuwa Tajiri Badili Fikra

Ukitaka kuwa tajiri inakupasa kuanza kufikiri kama matajiri wanavyofikiri.

[Soma : Mambo Ambayo Matajiri na Masikini Wanafanya Tofauti ]

Ukishapata ufahamu juu ya tofauti hizo achana na fikra na mbinu zako za mwanzo kuhusu mafanikio na anza mara moja kufuata na kuiga kile ambacho matajiri na waliofanikiwa wanafikiri na kufanya.

Utajiri ni sayansi,ikiwa na maana kuwa unaweza ukajaribu na kuona matokeo yale yale kila mara ukirudia jaribio lile lile katika mazingira yanayofanana.

Kutajirika ni matokeo ya kisayansi,kama utafanya vilevile kama ambavyo matajiri wamefanya kwa kufuata kanuni na nidhamu ileile ambayo wamefuata basi ni wazi kuwa utafanikiwa.

Tafuta Mtu wa Mfano wa Kuigwa

Kwanza tafuta watu matajiri ambao wamefanikiwa katika maisha kwa kuwa na matajiri. Oredhesha kama majina matano kwa kuanza yanatosha. Unaweza ukachagua wawili katika hao ambao ni wakimataifa na watatu waliobaki kutoka nchini kwako au mji unaoishi na hata katika familia au eneo lako la kazi. Kisha orodhesha maeneo ambayo unafikiri wamefanikiwa sana kifedha na mali nyingine kwa kila mmoja.

Fanya Utafiti Juu ya Mafanikio Yao

ukitaka kuwa kuwa tajiri fanya utafiti

Fanya utafiti wa maisha yao kuhusu namna ambavyo wamefanya kufikia mafanikio hayo,wengine wanaweza wakawa wamepitia njia zisizofaa,chagua zile ambazo ninafuata maadilina sheriaza nchi.

Fuatilia kuona ni watu gani wanaandamana nao na wanaongea na kufanya vitu gani pamoja.

Wameanzaje biashara ambazo wanafanya na wamekumbana na changamoto zipi katika njia yao ya kufikia mafanikio?

Kwa kila mtu mmoja uliyemuorodhesha jaza taarifa hizi. Soma kuhusu maisha yao binafsi na biashara.

Ukiweza kukutana uliza ni jinsi gani imewachukua kufika walipofika. Mwambie kuwa yeye ni mtu wa mfano kwake na ungependa ufanikiwe kama yeye. Omba akupe mbinu za mafanikio alizotumia.

Bila shaka kwa kumuhoji muhusika utapata habari nyingi zitakazokusaidia katika kubadiri fikra zako.

Fanya Maamuzi ya Kuanza Mara Moja

Ukitaka Kuwa Tajiri-Amua sasa

Fanyia kazi matokeo ya utafiti wako. Mafanikio yakuja kwa kufanya, na sio kujua peke yake.

Mojawapo ya tabia mabzo utagundua toka katika utafiti wako ni kuwa watu wenye kufanikiwa wana tabia ya kufanya maamuzi mara moja na kuanza kufanya kile wanachokifahamu na kuamini.

Wakati masikini wanatabia ya kuchelewa kufanya maamuzi na hatimaye kuacha kabisa.

Tengeneza mfumo wako kutokana na jinsi ambavyo umejifunza toka kwa watu uliowafanyia utafiti au chagua mfumo wa mtu mmojawapo na anza kufanya kama ambavyo amefanya ukiongezea ubunifu juu yake,ili mradi huhami katika mbinu kuu. Msemo wa kiswahili unaelezakuwa “Akili ya mwenzako,ongeza na za kwako”.

Soma Zaidi Kuhusu Watu Waliofanikiwa na Matajiri na Mbinu Zao

Endelea kusoma zaidi juu ya matajiri,fikra zao na mbinu zao. Kusoma vitabu vya kujielimisha ni mbinu mojawapo ambayo matajiri wanafanya na masikini hawafanyi.

Soma pia kuhusu elimu ya biashara na uongozi wake kama ambavyo matajiri wanafanya.

Jiunge na makundi na vyama vya matajiri ili uweze kujifunza zaidi na kufanikiwa.

 

 

Mwisho: Siri Ipo Katika Kufikiri na Kufanya Katika Namna Fulani:

Fikra peke yake hazitoshi,kufanya ndiko kunakokamilisha mipango yako ya mafanikio.

Unatakiwa kufanya kwa namna Fulani na kwa jinsi ile ile kama ambavyo imefanikiwa na wengine katika kuleta matokeo yaleyale waliyoyapata wengine.

Kumbuka kuwa utajiri ni matokeo ya sayansi,unatakiwa kufahamu vitu vinavyohitajika (inputs),taratibu na masharti ya kuzingatiwa (rules) na mfumo (system).

Ainisha vitu hivi vitatu katika kila wazo lako la biashara au kazi ambavyo vitakuletea matokeo unayo yahitaji yaani kuwa tajiri.

Tupe mtazamo wako katika mada hii juu ya kubadili fikra na kuwa tajiri. Tupe mbinu zako zinazofanya kazi kwako au kwa mtu mwingine. Andika katika sanduku la maoni chini ya makala hii.

Asante kwa kusoma na kushiriki kwa

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment

2 Comments

 • Ninashukuru sana kwa mashauri yenu mazuri. nina tumaini yana weza kunisaidia sana, ninapopata nafasi yaku elekezwa zaidi. Kwakweli mimi nina hitaji sana mashauri namaelekezo zaidi kutoka kwenu, ili nifikie maono niliyo nayo. mimi ni Paster, nakaa inchini congo katika mjii wa Goma DRC, Kwaupande wangu naona Nimejaliwa kipaji kizuri na Mungu chakuhubiri, kifundisha Neno la Mungu ipasavyo,na matokeo makuu katika maombi, nina mwamini Mungu, natena naaminia vipaji vizuri alinipa,pia nina furaha nabii yakuvitumia. ila katika mawazo yangu sitaki umasikini kabisa katika maishayangu na kanisani. ingawa kupitia halingumu ya inchi yetu umaskini naona unazidi kuni shambulia kabisa, ila ninapo jaribu kulinganisha wito na kipaji nilichopewa na Mungu, naona havilingane kabisa na maisha magumu ninayo pitia. pia maono ninayo yakuinua kipaji hiki sija mupata mtu wakaribu nasi aliye inuka hapa mjini anayeweza kuni elekeza.kwahiyo nina furahasana kugundua mashauri yenu mazuri namhimu kwangu,kwamtandao.kwahiyo naomba mashauri.

  • Mchungaji Bisimwa,
   Asante kwa kusoma na kufuatilia mada zetu to Congo.
   Ulimwengu una utajiri wa kutosha. Na jambo kubwa la kufahamu ni kuwa utajiri na umasikini unaanzia katika kufikiri kwetu. Anza kufikiri kitajiri leo kwa kuona nafasi za maendeleo katika jamii unamoishi. Soma juu ya watu wengine waliofanikiwa,ongea nao na fahamu vitu gani watu hawa wanafanya kuwawezesha kufika walipo. Ukishafahamu basi na wewe uanze kufanya kama wao.

   Mawazo pamoja na vitendo vinaleta mafanikio.

   Ukitaka kuwasiliana zaidi juu ya kuufukuza umasikini na kuleta neema katika maisha yetu. Tuwasiliane zaidi katika barua pepe (florensk@gmail.com) ili tubadilishane mawazo na uzoefu.

   Pia endelea kusoma mada zetu zinazokuja. Asante