Fedha na Uchumi

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Mafuta ya Gari

mafuta-ya-gari

Niwazi kuwa bei ya mafuta zimekuwa zikipanda kila siku.

Uchumi wa familia nyingi umekuwa ukiathiriwa  na bajeti za magari. Kwasababu ukiwa na gari ni lazima litatembea. Hivyo bajeti za magari zimekuwa kipaumbele.

Ndio maana sasa inakuwa ni kitu cha muhimu kwa wamiliki wa magari kufikiria namna tofauti za kupunguza matumizi katika magari yao na hivyo kuokoa fedha kwajili ya mahitaji mengine ya kifamilia au binafsi.

Kwa bahati nzuri, kuna njia nyingi za kuokoa kiasi kikubwa cha fedha bila hata ya jitihada kubwa toka kwako mmiliki au muendeshaji:

 

1. Panga safari zako ili kupunguza kilometa unazotembea
Panga safari zako zote na uziunganishe pamoja. Kama unaenda kazini kila siku na unahitaji kupeleka watoto shuleni,basi panga hizo zifanyike katika safari moja badala ya kila moja peke yake.

Fikiria kutembea badala ya kuendesha gari kwa safari za karibu. Ni nzuri kwa afya pia.

 

2. Pasha Moto Gari lako kwa muda mfupi tu

Huhitaji kupasha moto gari lako kwa muda mrefu unapowasha asubuhi kama wengi wanavyofikiri na kufanya.

Magari ya kisasa yanahitaji sekunde 30 tu za kupshwa moto.

Kuacha ingini iwake bila kazi kwa dakika kadhaa tu unapoteza mafuta mengi bila sababu na kuchafua mazingira kwa kutoa gesi ya ukaa.

 

3. Jaza mafuta mapema asubuhi  au jioni
Nunua mafuta wakati wa asubuhi au jioni. Mafuta yanakuwa mazito zaidi wakati huu ambapo joto liko chini.

Hivyo unapata mafuta mengi zaidi kuliko wakati wa mchana.

 

4. Endesha na Ongeza Mwendo Taratibu.

Kuendesha gari kwa kasi kunaweza kukawa kunatia raha lakini kunatia hasara mfukoni mwako.

Kuendesha gari kwa kasi ndogo na kuongeza mwendo taratibu(kukanyaga mafuta taratibu)  kunatumia mafuta vizuri.

 

5. Kufuatilia Wakati na jinsi Kupiga Breki
Kufunga breki kwa haraka kunakula mafuta kwa wingi na pia kunamaliza breki zako.

Acha umbali wa kutosha katiyako na gari la mbele unapokuwa kwenye foleni za magari. Hilo litakusaidia kupunguza mwendo taratibu.

 

6. Kuzima injini
Zima injini kila mara unaposubiri mtu. Usiache gari likiwaka bila kazi. Mafuta mengi yanatumika injini inapozunguka gari likiwa limesimama.

Lakini pia moshi unaotoka ukiwa umesimama unasababisha uchafuzi mkubwa wa hewa.

 

7. Funga vioo vya gari kupunguza ukinzani wa upepo

Kuendesha gari madirisha yakiwa wazi kunaongeza ukinzani katika gari lako na hivyo gari kuhitaji nguvu zaidi. Hivyo kutumia mafuta zaidi. Ikiwezekana funga vioo vya gari unapoendesha.

Pia punguza mizigo ndani ya gari lako. Mizigo inaongeza ulaji wa mafuta.

 

8. Epuka vituo vya mafuta karibu na barabara kuu
Kituo cha kwanza mafuta ambayo utakutana nacho barabara kuu ni wazi kitakuwa na bei za juu za mafuta.

Angalia vituo vya mafuta katikati ya mji ili kupata mafuta kwa bei nafuu.

 

9.  Angalia Upepo wa Matairi Yako
Kuendesha gari ukiwa na matairi yenye upepo kidogo husababisha kuisha kwa haraka na kuongezeka kwa matumizi ya mafuta.

Matairi yenye upepo wa kutosha hupunguza msuguano na barabara hivyo kusababisha matumizi mazuri ya mafuta.

 

10. Rekebisha Injini Mara kwa Mara
Injini ya gari inahitaji kuangalia na kufanyiwa marekebisho mara kwa mara. Injini inayopata huduma hutumia mafuta vizuri.

Badilisha oili ya enjini kila mara unapopeleka gali kufaniwa matengenezo(“Service”) .

 

11. Mabadiliko ya Chujio
Angalia chujio za mafuta (“Fuel Filter”)  na hewa (“Air filter”) mara kwa mara – hasa kama unaishi au kusafiri maeneo yenye vumbi.

Chujio safi zinasababisha gari kwenda kasi zaidi na kutumia mafuta vizuri.

 

12. Matumizi sahihi Oil
Tumia oili sahihi na safi kwenye gari lako.

Angalia kitabu cha muongowa gari lako kama huna uhakika.

 

13. Zima A / C
AC inaongeza matumizi ya mafuta katika gari lako. Kama inawezekana ,zima AC unapokuwa unaendesha.

Paki gari lako katika kivuli ili kupunguza joto ndani ya gari. Hata kama utawasha AC utasaidia AC kutotumia mafuta mengi.

 

14. Chagua Njia nzuri
Kila inapowezekana, chagua njia fupi na yenye vizuizi vichache vya barabarani.

Njia yaenye foleni ndefu itasababisha matumizi makubwa ya mafuta.

 

15. Nunua  au Endesha Gari Lenye Kutumia Mafuta Kidogo

Kufikiria kununua na kuendesha gari lenye matumizi mazuri ya mafuta. Kwa miji ambayo ina foleni ndefu kama Dar es Salaam,Tanzania au Kampala, Uganda magari madogo chini ya cc 1000 ni chagua  bora zaidi.

Baadhi ya magari ya aina hii yana uwezo wa kwenda hadi kilometa 40 kwa lita moja ya mafuta.

 

Kwa kufuata muongozo huu unaweza kupunguza matumizi ya mafuta katika gari kwa kiasi kikubwa.

Fedha iliyookolewa ni sawa na kipato kingine katika mfuko wako au familia.

 

Kama una njia nyingine kusaidia kupunguza matumizi ya mafuta ya gari, basi ongeza katika kisanduku cha “Comments ”  hapo chini.

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment

1 Comment