Sayansi na Teknolojia

Kemikali za Furaha Mwilini:Dopamine,Endorphin,Oxytocin na Serotonin

Kemikali-za-Furaha-Mwilini

Binadamu ana aina mbili za mfumo ya fahamu: Mfumo wa Limbic na Cortex.Mifumo hii humfanya binadamu aishi na hulinda mfumo wa seli za DNA.

Mfumo wa limbic huzalisha kemikali ambazo huuambia mwili kipi ni kizuri au kibaya. Kunapotokea kitu kizuri ubongo unazalisha kemikali nne(Kemikali za Furaha Mwilini): Dopamine, Endorphin, Oxytocin na Serotonin na kunapokuwa na kitu kibaya kemikali ya hisia mbaya: Cortisol huzalishwa

Kemikali za Furaha Mwilini

Dopamine, Endorphin, Oxytocin na Serotonin ni kemikali ambazo zinamfanya binadamu kujisikia vizuri na hutengenezwa mwilini kutegemeana na vichocheo fulani. Kila kemikali hii husababisha hali ya kujisikia vizuri.

Kemikali hizi zote zinatengenezwa mwilini na zinaathiri hisia zetu ambazo pia huathiri matendo na tabia zetu.

Kemikali hizi zinaweza zikadhibitiwa kiwango chake cha kuzalishwa mwilini kama ambavyo tutazungumzia hapa,hivyo kutoa mwanya wa kila mtu kuweza kuongoza hisia na tabia zake.

Kemikali hizi zinazalishwa mwilini kutokana na mwongozo wa ubongo na zinakufanya ujisikie vizuri,lakini kemikali hizi hazikai mwilini muda wote hivyo zinapoisha unahitaji vichocheo fulani ili zitengenezwe tena.

#1. Dopamine

Kemikali-za-Furaha-Mwilini-dopamine

Hujenga hali ya furaha juu ya kutafuta kitu na kukipata, “Ohh! nimefanikiwa!” ni mojawapo ya viashilia vya furaha hii na  ni kazi ya dopamine. Inakufanya uruke kwa furaha unapofikia lengo.

Mamalia yeyote akiwemo binadamu hutengeneza dopamine pale anapokaribia kupata matokeo mazuri. Simba mfano ananpomfukuza swala na akakaribia kumshika dopamine huongezeka mwilini ambayo humuongezea ali ya kufikia mafanikio.

Hali kadhalika kwa binadamu,tunapokuwa na tunakaribia kutimiza lengo au jambo zuri ubongo wa mwanadamu huzalisha kwa wingi kemikali ya dophamine mwilini na humfanya binadamu kujisikia vizuri na huongeza nguvu za kukufanya ufikie mafanikio.

Dopamine inakuongezea ali ya kutafuta,iwe ni kupata digrii katika masomo au kufikia lengo katika kazi na biashara. Inakupa uwezo wa kuhimili ili ufikie haja au mahitaji yako. Je umewahi kucheza mchezo katika kompyuta au simu na ukakaribia kushinda? au ukashindwa? Kuna hali ya msukumo ya kutaka kuendelea kucheza mpaka ushinde. Hii ni kazi ya dopamine.

#2. Endorphin

Kemikali-za-Furaha-Mwilini-Endorphin

Hutengeneza ganzi katika mwili ambayo itakufanya usijisikie maumivu.

Maumivu ya mwili husababisha kuzalishwa kwa endorphin. Kemikali hii hutengenezwa wakati wa hatari kwa asili. Lakini inawezwa kutengenezwa kwa mazoezi na kucheka au kulia.

Katika hali ya hatari au shida kemikali hii inawasaidia wanyama akiwemo binadamu kuweza kuhimili maumivu mpaka wanapokuwa salama au kupata nafuu au msaada.

Ukiwa katika shida unaweza ukakimbia bila viatu katika mawe au miba bila kusikia maumivu,mpaka baadae wakati kemikali hii ipokuwa imepungua.

Kemikali hii huzalishwa wakati wa shida tu na sio wakati wote. Kama ingewezekana kuwa nayo wakati wote basi binadamu angekuwa na uwezo wa kushika moto bila ya kuhisi maumivu yoyote.

Kucheka na kufanya mazoezi ya mwili kunazalisha endorphin pia kwa njia ambayo binadamu ana maamuzi nayo.

#3. Oxytocin

Kemikali-za-Furaha-Mwilini-Oxytocin

Hutengeneza hisia za kujisikia mwenye amani na usalama mbele ya wengine.

Oxytocin inakusaidia kumwamini mwenza wako katika mahusiano na inajenga mshikamano kati yenu.

Imani juu ya mtu au kitu huamsha utengenezwaji wa kemikali ya oxytocin. Kemikali ambayo inafanya mtu awe na mshikamano wa karibu kihisia na mwingine anayemwamini.

Oxytocin ni muhimu sana katika mahusiano ya aina yoyote yakiwemo ya mapenzi. Ifahamike pia kumwamini mtu asiyeaminika ni hatari kwako. Uaminifu unapovunjwa hukufanya utengeneze kemikali nyingine mbaya mwilini. Na hili linakufanya ujenge umbali na mwenza wako.

Hili ni muhimu kwa wapenzi kufahamu. Uwepo wa Oxytocin mwilini kunaongeza muunganiko kati ya wawili hao na kunajenga uaminifu kati yao. Kila unaposhindwa kumwamini mweza wako unapunguza kiasi cha kemikali hii na hivyo utajisikia vibaya.

Unaweza ukachochea uzalishaji wa Oxytocin kwa kutengeneza uaminfu kwa makusudi. Panga mambo ambayo mwenza wako atatimiza,na hivyo ataongeza uaminifu kwako, njia hii itaongeza kuamini na kuzalisha oxytocin na kukufanya ujisikie vizuri.

#4. Serotonin

Kemikali-za-Furaha-Mwilini-Serotonin

Hutengeneza hisia za kuheshimiwa na wengine,au hali ya kujisikia vizuri kwa mafanikio uliyonayo.

Kujiamini kunaamsha uzalishaji wa serotonin mwilini. Kufanya mambo ambayo yatakufanya uheshimiwe na watu huzalisha serotonin na hivyo huenda ikamfanya mtu arudie kufanya mambo haya kila anapohitaji kujisikia vizuri kwa kutengeneza kemikali hii

Isipodhibitiwa vizuri mahitaji ya kemikali mwilini yanaweza kumfanya mtu kufanya mambo fulani kupita kiasi na uwezo.

Mfano mtu anapotoa msaada kwa wasiojiweza, ni kitendo kinachompa heshima katika jamii na inamfanya ajisikie vizuri. Kila mtu anahisi vizuri anapotoa kwasababu mwili wetu unatengeneza serotonin.


Namna ya Kuchochea Uzalishwaji wa Kemikali za Furaha Mwilini

Zifuatazo ni namna ya kuamsha uzalishaji wa kemikali za furaha mwilini zinazomfanya binadamu kujisikia vizuri:

 1. Vichocheo Vya Dopamine

Dopamine inasaidia kutengeneza nguvu za ziada ili kupata matokeo tunayoyataka-Inapandisha molali ya kufanya jambo.

Tunaweza kuchochea uzalishaji wake kwa kufanya yafuatayo:

 • Kuchukua Hatua Ndogo Ndogo
  Kwa kugawa kazi kubwa katika vipande vidogo vidogo inasaidia kazi kufanyika kirahisi kwa kuwa ni fupi na ni rahisi kufikia lengo dogo kuliko kazi yote.
  Dopamine inazalishwa kukuwezesh akukamilisha sehemu ndogo ya kazi na hatimaye kazi yote kuisha.
 • Jipongeze
  Jipongeze kwa kufikia mafanikio na kutakufanya ujisikie vizuri
 • Panga na Chukua Hatua
  Weka malengo ya kufanya mambo kadhaa kila siku na kukamilisha

 2. Vichocheo Vya Endorphin

Kwa asili kemikali hii huchochewa na maumivu mwilini. Lakini inaweza pia kuchochewa na baadhi ya mambo:

 • Kucheka
  Kucheka kwa kweli ambako kunakufanya tumbo liume au uso uume
 • Kulia
  Kulia kunachochea kutengenezwa kwa endorphin. Pia kunasaidia kutoa msongo wa mawazo na kukufanya ujisikie vizuri.
 • Mazoezi
  Kufanya mazoezi kunasaidia kutengeneza endorphin. Mazoezi ambayo yanakufanya usikie maumivu kidogo yanaleta majibu mazuri zaidi.

3. Vichocheo Vya Seratonin

Kwa asili setatonin inazalishwa pale mtu anapojisikia kuwa juu au mkubwa kuliko wengine. Lakini kuna jinsi nyingine zenye kuleta matokeo sawa:

 •  Kufurahia Pale ulipofikia:
  Ukifahamu kuwa mafanikio si lazima kuwa juu ya wengine wote na wakati ungine ni vizuri kuwa chini itakufanya ujisikie vizuri katika ngazi yoyote.
 • Angalia Ushawishi wako
  Bila kuonyesha majivuno na majigambo unaweza ukajisikia vizuri kwa kuaona jinsi ambavyo wengine wamefaidika kwa msaada wako hata kama hakuna shukurani zinazotolewa moja kwa moja.
 • Jiridhishe Mwenyewe:
  Usitegemee sana watu kuona na kupongeza matendo na matokeo yako mazuri. Kuwa mtu ambaye unajipongeza binafsi na ujiridhishe. Kwa namna hii utajisikia vizuri kila mara kwa matendo na matokeo yako.

4. Vichocheo Vya Oxytocin

Wazazi wa watoto na watoto wenyewe huzalisha kemikali hii wakati wa uzazi na huwafanya kuwa na mvuto wa kuwa pamoja. Hii ni zawadi ya wazazi wanawake katika malezi ya watoto. Akina baba nao wanaweza kujenga mvuto huu kwa kuwa karibu na watoto nakuwashika na kuwakumbatia mara kwa mara kwa upendo sio tu kama roboti.

Namna nyingine ya kutengeneza Oxytocin na uaminifu ni kwa kufanya yafuatayo:

 • Jenga uaminifu:
  Kuwa na tabia ya kuwaamini watu. Kama wengine wakifahamu kuwa wanaweza kukuamini basi wanakufanya uwaamini pia.
 • Kuwa na Watu Waamnifu
  Uaminifu unahitaji muda kukua. Kuwa na marafiki ambao wanaaminika na mpe mwenza wako nafasi ya kufanya mambo ambayo yatakufanya umuamini hasa kama uaminifu wake umevunjika.
 • Masaji na Kukumbatiana
  Kufanya masaji ya mwili kunakufanya ujisikie vizuri na kunasaidia kutengeneza oxytocin. Kukumbatiana na mtu pia kunaongeza kemikali hii mwilini.Kukumbatia watoto kunajenga mshikamano kati ya mtoto na mzazi kwa kuamsha uzalishaji wa oxytocin
 • Kufanya Mapenzi

  Kufanya mapenzi na kufika kileleni kunazalisha oxytocin na kunaongeza mshikamano na kuaminiana.

  Imefahamika kuwa wapenzi humaliza ugomvi wao mara baada ya kufanya mapenzi na hivyo baadhi yao wamekuwa wakitumia kama njia ya usuluhishi. Jaribu kama inakuhusu na tupe matokeo yake.

 

Je, Kuhusu Kemikali zinazokufanya Ujisike Vibaya?

Katika upande wa pili wa shilingi,kuna kemikali zinazokufanya ujisikie vibaya: Cortisol
Cortisol inakufanya ujisikie vibaya. Inatoa ishara kwa wanyama kuhusu jambo baya. Kemikali hii ipo nasi siku zote kwani kuna mambo yanayotishia usalama wetu kila siku katika maisha yetu.

Kemikali hii inaleta athari kubwa kama kunakosekana kemikali za furaha mwilini mwako.

Je,Umewahi kulala usiku na ukahisi kuna mtu anatembea nje ya nyumba karibu na dirisha lako au mlango? Sikiliza mwili wako katika wakati kama huu. Utasikia kemikali hii inavyopita katika kila mshipa wa mwili wako.

Kemikali hii ni nzuri kama zilivyo zile nyingine kwa kuwa inakupa tahadhari ili uchukue hatua ya haraka juu hatari iliyo mbele yako.

Chagua Hisia Zako:

Kwa kujua uwepo wa kemikali za furaha mwilini na jinsi zinavyozalishwa kunakusaidia wewe kuamua juu ya hisia zako na matendo yako kwa faida zaidi.

Chagua kuzalisha kemikali ipi na wakati gani kwa kazi ipi na kwa matokeo unayoyategemea.

 

&n

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment