Michezo

Kombe la Dunia 2014: Timu 5 Bora za Kuangaliwa

Kombe la Dunia 2014 limeanza kwa kasi. Tumeshuhudia baadhi ya timu kubwa kama Hispania ikipokea kipigo cha aibu cha 5-1 toka kwa Uholanzi. Lakini mambo bado machanga,bado kuna nafasi ya kubadilika.

Zifuatazo ni timu tano ambazo zina uwezo mkubwa wa kufanya vyema na hata kuchukua ubingwa.

Orodha hii inatokana na nafasi zao katika mpangilio wa FIFA viwango vyao ambavyo vimeoneshwa siku za karibuni.

 

1. Hispania

spain_national_team
Karibu mashindano nane yaliyopita kabla ya kunyakua kombe 2010 Afrika Kusini wamekuwa wakiishia robo-fainali.

Kwa miaka minne yote toka 2010 wamebakia nafasi ya kwanza kulingana na viwango vya FIFA hivyo wanapewa nafasi kubwa kushinda tena au kufika mbali katika mashindano.

Ina wachezaji mahili na wenye viwango vya juu kabisa kama Iker Casillas(Golikipa), Sergio Ramos na Gerard Pique Jordi Alba,David Villa, Fernando Torres, Diego Costa na wengine.

 

2. Brazil

brazil_national_team
Wakiwa chini ya Mwalimu Scolari kama washindi wa FIFA Kombe la dunia 2014 na waandaaji wa mashindano ya mwaka huu, Brazil wanapewa nafasi kubwa.

Pia wameeanza vizuri kwa kuwafunda Croatia 3-1 katika mechi ya ufunguzi.

Wakiwa na wachezaji maarufu kabisa duniani na wenyr umri mdogo ni wazi watakuwa tishi katika mashindano ya mwaka huu.

Wakiwa na washambuliaji hatari kabisa kama Neymar ,Oscar, Dani Alves na Zenit upinzani mkubwa kabisa.

Golikipa veterani Julio Cesar atahakikisha hakuna mipira inayogusa nyavu akiwepo golini.

 

3. Uingereza

Equipe Angleterre
Wakiwa katika nafasi ya 10 na wakiwa wamekosa kombe kwa miaka mingi toka wachukue ubinwa mara moja mwaka 1966 ni wazi watagombana kufa na kupona kugombe kombe mwaka huu.

Wayne Rooney na wenzake wenye uzoefu mkubwa kama Gerrard,Frank Lampard, Daniel Sturridge ,Jack Wilshere, Alex Oxlade-Chamberlain na Ross Barkley kama kawaida watagombana moyo-nje kuhakikisha ushindi.

 

4. Ujerumani

german_national_team1
Mabingwa mara nne Ujerumani japo ina wachezaji wake wengi ambao hawatashiriki bado wanapewa nafasi za juu kushinda na kutoa upinzani.

Wachezaji wake mahiri Manuel Neuer, Thomas Muller, Toni Kroos, Boateng, Lahm, Julian Draxler na Podolski ushindi kwao ni jambo la kutegemewa.

KumbukaThomas Muller alishinda Kiatu cha Dhahabu cha Adidas mwaka 2010 kwa kupachika magoli 5 katika mashindano, hivyo tegemea makubwa toka kwake mwaka huu pia.

 

5. Ufaransa

france_national_team
Timu ya kocha Deschamp Dider ipo katika nafasi ya 17 katika msimamo wa viwango vya FIFA wana uzoefu na mashindano na wanapata nafasi ya kutoa ushindani na kugombea ubingwa.

Baada ya kusuasua siku za karibuni timu hii imerudi katika kiwango na bira shaka itatisha mwaka huu.

Kikos chake kina wachezaji muhimu kipa Hugo Lloris , rearguard , Patrice Evra, Laurent Koscielny , Raphael Varane, Paul Pogba

Washambuliaji hatari kama Karim Benzema na Olivier Giroud wana uchu mkubwa na nyavu za wapinzani wao.

Kuna timu nyingi nyingine ambazo zinauwezo mkubwa na hizi ni chache tu. Wewe una maoni yapi? Toa timu zako 5 kwa jinsi ya uchambuzi wako.

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment