Michezo

Kombe la Dunia 2014 : Timu Kali za Kuangalia

worldcup2014-Brazil

Kombe la dunia 2014 limefika hatimaye na ufunguzi umeanza kwa wenyeji Brazil kuwa bamiza Croatia mabao 3-1 juni 12 mjini Sao Paulo.

Lakini fahamu timu zenye mvuto mkubwa katika mashindano haya hasa kwa kuangalia nafasi ya ubora duniani kwa vigezo vya FIFA na viwango vya wachezaji walionao.

Ukiachia majina makubwa kama Brazil na Hispania kuna timu nyingine zenye soka nzuri na utafurahia kuangalia wakicheza dimbani.

1. Argentina

argentina_national_team
Argentina katika miaka ya karibuni imekuwa ikijitahidi sana katika mashindano mbalimbali pengine bila mafanikio ya kutosha. Wengine wamekuwa wakilaumu kuwa wanategemea sana majina ya wachezaji wakubwa kama Lionel Messi, na wakati amekuwa hafanyi vizuri sana akiwa katika timu yake ya taifa kama vile anavyofanya katika klabu.

Hata hivyo mambo yamebadilika sana kwenye timu hii kwa sasa, kuna kujiamini ndani ya timu kwani kuna vipaji vingine vipya vinaonekana kuibuka kama vile Di Maria na Mascherano. Hivyo kuna mategeneo makubwa ya kandanda safi katika mashindano haya toka kwao.

Wachezaji wa Kuangaliwa:

Lionel Messi, Di Maria na Mascherano

 

2. Ureno

portugal_national_team
Ureno, kama wote tunavyojua kuwa ina kikosi kizuri, wachezaji wengi wa viwango vya juu duniani kama Ronaldo, na Pepe wamo katika timu hii.

Ni wazi tunategemea ushindani mzuri na kandanda safi toka kwao.

Wachezaji wa Kuangaliwa:

Cristiano Ronaldo,Pepe,Nani

 

3. Colombia

columbia_national_team

Naweza kukuambia kuwa hakuna timu moja katika mashindano haya ambayo itaombea kucheza na Colombia, kwani ni timu kali sana.

Wana wachezaji wenye vipaji vikubwa sana katika soka na washambuliaji bora kabisa mfano Falcao.

Ni timu iliyojipanga sana na yenye kucheza kwa maelewano. Tehgemea burudani tosha na upinzani mkubwa kwa timu nyingine.

Wachezaji wa Kuangaliwa:

Falcao, Redy Guarin & James Rodriguez

 

4. Uruguay
uruguay_national_team
Uruguay ina wachezaji wazuri kama wakicheza katika viwango vyao. Si ajabu wakafika robo fainali hata zaidi.

Na kwasababu mashindano yanafanyika Amerika ya Kusini,barani kwao hali ya hewa inawasaidia zaidi.

Wanakikosi stahimilivu na wenye stamina kubwa.

Kama miaka mingine timu pinzani zisitegemee mteremko kwa Uruguay.

Wachezaji wa Kuangaliwa:

Luis Suarez,Diego Forlan,Diego Lugano,Edinson Cavani

 

5. Ubelgiji

belgium_national_team
Ubelgiji ni nchi yenye mvuto na yenye wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu.

Hakuna nafasi ya kusema kuwa eti utawashinda kirahisi. Wachezaji wao wote ni wataalamu na wenye kucheza kiwango cha mataifa. Lukaku na Kompany ni baadhi tu ya majina ya kutisha.

Watu wanaiweka Ubelgiji katika nafasi za juu kabisa kuchukua kombe mwaka huu.

Wachezaji wa Kuangaliwa:

Vicent Kompany, Eden Hazard Na Romelu Lukaku
6. Uholanzi

Pays Bas
Kwa miaka mingi Uholanzi imekuwa na timu nzuri sana ya Taifa na wamekuwa wakifanya vizuri sana katika mashindano makubwa kama haya.

Waliingia fainali na kufungwa na Hispania katika fainali za mwaka 2010 Afrika ya Kusini.

Huwezi kujua wataishia wapi katika mashindano haya.

Wachezaji wa Kuangaliwa:

Arjen Robben, Robin van Persie , Wesley Sneijder na Klaas-Jan Huntelaar.

 

 7. Uswisi
switzerland_national_team

Uswisi ambao waliingia kirahisi katika mashindano haya pia ni timu nzuri sana. Ni timu yenye mbinu za kushambulia. Ni timu yenye wachezaji wenye moli wanapokuwa mchezoni na bila shaka ni mojawapo ya timu zitakazovutia wengi katika fainali hizi

Wachezaji wa Kuangaliwa:

Granit Xhaka, Xherdan Shaqiri na Gokhan Inler

 

8. Urusi

russia_national_team
Ni timu yenye kucheza kwa nguvu, na umoja.

Ni timu inayofikiria ushindi kwenye kila mechi wanayocheza.

Si ajabu ikifika mbali katika mashindano ya mwaka huu.

Wachezaji wa Kuangaliwa:

Igor Akinfeev (Golikipa),Alexander Kerzhakov , Roman Shirokov Na Vasiliy Berezutskiy

 

9. Japan

japan_national_team

Japan ina wachezaji wenye vipaji sana, na wenye umoja na hushambulia kama nyuki.

Kila mchezaji anashirikishwa uwanjani.

Japo ni taifa changa katika soka lakini ni timu yenye uwezo wa kutoa upinzani kwa timu yoyote kubwa kama Brazil na Ujerumani.

Wachezaji wa Kuangaliwa:

Keisuke Honda, Shinji Kagawa, Shinji Okazaki

 

10. Marekani

usa_national_team
Marekani inakuja kwa kasi na inakua kila mwaka. Kama katika michezo mingine Marekani ni maarufu kwa kusaka vipaji na kuvitumia vyema hasa katika mashindano ya kimataifa kama haya.

Hivyo imwkuwa timu yenye kutoa ushindani mkubwa kwa wapinzani hata matifa makubwa yaliyobobea katika soka. Matokeo yake yamekuwa yakiwashangaza wengi. Angakia nini wanafanya mwaka huu.

Wachezaji wa Kuangaliwa:

Matt Besler (Mlinzi), Tim Howard, Landon Donovan na Michael Bradley

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment