Biashara na Ujasiriamali Fedha na Uchumi Mafanikio

Hatua 10 za Kuanzisha Biashara Yenye Mafanikio

new_business_1

Watu wengi wamekuwa wakisita kuanza biashara kwasababu taratibu za kufuata zinaonekana kuwa ni ndefu sana. Lakini siri ya mafanikio imesemwa kuwa ipo kwenye “KUANZA”.

Kuanzisha biashara inahusisha mipango, na kufanya maamuzi muhimu ya kifedha na kukamilisha mlolongo wa taratibu za kisheria.

Mara baada ya kufanya hatua ya kwanza nyingine zitajipanga zenyewe.

 

Zifuatazo ni hatua10 kukusaidia kupanga, kuandaa na kusimamia biashara yako:

 

1. Mpango wa Biashara (Business Plan)
Imekuwa ikisemwa “Kama huna mipango basi unapanga kushindwa”. Hivyo kama una mipango ya kuanzisha biashara basi unahitaji Mpango wa Biashara.

mpango wa biashara ni hati ambayo inaelezea jinsi ya biashara itakuwa kukimbia.

Mpango wa biashara ni muhimu kwa mafanikio ya biashara yako. Mpango wa biashara huonyesha dira ya miaka 3-5 mbele na huonyesha njia ambayo Kampuni inatarajia kuchukua kukua kimapato

Mwongozo huu utasaidia kukupa ramani ya jinsi gani ya kuanza na kuendesha biashara yako kwa mafanikio.

 

2. Pata Elimu na Mafunzo ya Biashara
Biashara nyingi hushindwa kwa sababu wamiliki wanakosa ujuzi na elimu ya biashara .

Kama nyanja nyingine za maisha ili kufanikiwa katika biashara unahitaji kujifundisha jinsi ya kuendesha na kukuza biashara.

Pata Mshauri katika biashara na tafuta msaada wa kitaalamu. Weka kando bajeti kwa ajili hiyo.
Soma vitabu ili kuboresha maarifa yako katika usimamizi wa biashara na mahesabu ya fedha.
Kuna faida kubwa kwa kujiandikisha katika masomo ya jioni ya biashara katika chuo cha biashara katika eneo unaloishi.

 

3. Kuchagua eneo kwa ajili ya Biashara yako
Eneo muafaka kwa ajili ya biashara yako ni muhimu sana.
Kama unauza bidhaa mfano,kuweka duka katika ghorofa ya 10 inaweza kuwa si sahihi, unapaswa kuangalia nafasi katika ghorofa ya chini ambapo watu wanaweza kuja kwa urahisi.

 

4. Kupata fedha kwa ajili ya Biashara yako
Unaweza hitaji kujiandikisha kupata mikopo katika benki.
Unaweza pia kuomba mkopo kutoka kwa rafiki au familia.
Kama una Mpango Biashara mzuri na wenye kushawishi kupata fedha inaweza kuwa rahisi.

Onyesha mpango wako kwa wakopeshaji fedha na unaweza ukafanikiwa.

Njia nyingine unaweza kuweka akiba kidogo kidogo kutoka katika vyanzo vyako vya sasa vya mapato mpaka mpaka itakapofikia kiwango cha kuanza biashara.
 5. Kuchagua Aina ya Biashara
Amua ni aina gani ya umiliki ni bora kwa biashara yako kati ya Umiliki Peke (Sole Propriatorship), ushirikiano (partnership), Kampuni (Limited Liability Company) au au Ushirika(Corporation).

Kuna athari za gharama katika uchaguzi wowote utakaofanya.
Kama wewe uko peke yako na hutaki shida katika usimamizi , basi unaweza ukahitaji kuwa Mmiliki Peke (Sole Propriatorship) .

Biashara aina ya Kampuni, Ushirikiano na Shirika huhusisha zaidi taratibu za kisheria na hutozwa kodi za juu zaidi.

Lakini ni machaguo pekee unayobaki nayo kama wamiliki ni zaidi ya mtu mmoja.

 

6. Usajili wa Jina la Bishara
Utahitaji kuandikisha biashara yako kwa msajili wa makampuni wa serikali.
Michakato mingene inayofuata itahitaji kutumia jina la biashara kama vile vuchapishaji wa vitabu vya biashara, vifaa vya kujitangaza na usajili wa kulipa kodi

 

7. Kujiandikisha kwa ajili ya Ushuru na kupata Nambaya Kulipia Kodi (TIN)
Utahitaji kuwa na Namba ya Mlipa Kodi ili kufanya aina yoyote ya biashara.
Mamla ya kodi itafungua akaunti kwa namba yako ya kodi ambamo malipo yako yote ya kodi yatahifadhiwa na kufuatiliwa.

 

8. Kutengeneza Nyaraka za kampuni
Utahitaji kutengeneza nyaraka za biashara. Vitabu vya ankara, mikataba na vitabu vya fedha.

Alama ya kampuni(Logo),Vicha vya barua(letterhead) na Maelezo ya Kampuni (Company Profile) vitakuwa miongoni mwa vitu muhimu.

Vifaa vya matangazo kama vipeperushi na kadi za biashara ni muhimu sana kuzingatia .

Usisahau tovuti ya kuonyesha huduma zako na bidhaa.

 

9. Kupata leseni za biashara
Unahitaji kupata leseni ya biashara kuwa na uwezo wa kufanya biashara yako. Hii inatolewa na halmashauri ya jiji lako au manispaa.
Watatahmini biashara yako ili kufuzu na baada ya hapo leseni itatolewa na unaweza kuanza kazi.

 

10. Kuelewa majukumu ya mwajiri
Jifunze taratibu za kisheria zinazohitajika katika kuajiri wafanyakazi.
Ujifunze sheria za kazi na masuala ya kisheria unayohitaji kufuata kama mwajiri.
Ufahamu juu ya masuala ya kodi ya zuio(Withholding Tax) na pensheni ni jambo muhimu sana.

Kama utafuata hatua tajwa juu basi ni wazi utafanikiwa na kuwa nauhakika bishara yakoitaenda vyema na kwa udhabiti mkub

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment