Michezo

Kumi bora ya wanasoka matajiri duniani

ronaldo-messi2-300x225

Mpira wa miguu umekua ni ajira kwa watu wengi duniani hususani vijana , wengi wametajirika kupitia mpira wa miguu kutokana na mishahara wanayolipwa na matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali.

Ifuatayo no orodha ya wachezaji wanaongoza kuwa na pesa nyingi duniani ikilinganishwa na wengine.

1.Cristiano ronaldo.(pauni 122mil.)

Mchezaji huyu  wa Real Madrid na raia wa Ureno anaongoza kwa kuwa na pesa nyingi huku akimiliki pauni milioni 122 katika akaunti yake, mapato anayoingiza kupitia mshahara na mikataba ya matangazo.

2.lionel messi.(pauni 120.5 mil.)

Mwanasoka huyu wa barcelona na raia wa Argentina anashika nafasi ya pili nyuma ya Cristiano Ronaldo, anamiliki pauni milioni 120.5 katika akaunti yake, ambayo ni malipo ya mshahara na makampuni mbalimbali ya michezo na vinywaji.

3.Samuel Eto’o.(pauni 70 mil.)

Ni mchezaji aliye maliza mkataba wake na Chelsea msimu uliokwisha na raia wa Cameroon, anashikilia nafasi ya tatu kwa wanasoka wenye pesa zaidi kutokana na mishahara na matangazo.mkongwe huyu aliyekwisha zichezea klabu kama Barcelona, Inter milan, Real madrid na Chelsea.

4.Wayne Rooney.(pauni 69 mil.)

Mwanasoka wa kiingereza anayeichezea klabu ya Manchester united ndiye anayeshikilia namba nne kwa wanasoka matajiri duniani, huyu ndiye mwanasoka anayelipwa zaidi Uingereza huku akiwa na mikataba ya kutangaza katika kampuni mbalimbali.

5.Ricardo Kaka.(pauni67.5 mil.)

Mchezaji huyu wa AC Milan ya Italia anashikilia namba tano katika orodha hii ya wachezaji wa soka matajiri zaidi duniani .vyanzo vyake vya mapato ni mshahara na matangazo mbalimbali.

6.Neymar dos Santos.(pauni 66 mil.)

Mchezaji wa Fc Barcelona na timu ya Taifa ya Brazil, anashikilia nafasi ya sita katika orodha hii kutokana na fedha za mishahara na matangazo mbalimbali.

7.Ronaldihno Gaucho.(pauni 64 mil.)

Mchezaji wa Atletico mineiro ya Brazil na Timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho Gaucho ndiye anayeshikilia namba saba katika orodha hii, huku vyanzo vyake vya mapato vikijulikana kama mshahara na matangazo.

8.Zlatan Ibrahimovic.(pauni 57 mil.)

Mchezaji huyu mwenye jina la utani Ibracadabra ndiye anayeshikilia namba nane katika orodha hii, ni mchezaji wa PSG ya Ufaransa na Timu ya taifa Sweden, vyanzo vya mapato ya Ibramovic ni mshahara,matangazo na biashara.

9.Gianluigi Buffon.(pauni 52 mil.)

Huyu ni mlinda mlango wa Juventus ya Italia na timu ya Taifa ya Italia, utajiri wake unafikia pauni milioni 52, kutokana na malipo ya mishahara, matangazo pamoja na biashara.

10.Thierry Henry.(pauni 47 mil.)

Mwanasoka wa Ufaransa na timu ya New york redbulls ya Marekani ndiye anayefunga orodha hii ya wanasoka matajiri duniani, Henry aliye wahi kuzitumikia klabu za Arsenal,Juventus,Monaco na Barcelona anaingiza pesa hizo kutokana na mshahara na matangazo ya michezo na vinywaji.

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment