Jamii

Madhara ya Mwezi Katika Hisia na Tabia za Binadamu:Kuna Ukweli?

madhara-ya-mwezi

Kwa miaka mingi imekuwa ikiaminika kuwa kuna madhara ya mwezi kwa binadamu na wanyama pia. Na kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya nafasi ya mwezi katika mzunguko wake na mwenendo wa tabia na hisia za binadamu.

Tafiti mbali mbali zinaonyesha uhusiano kati ya vitu hivi viwili ukiwemo ule iliyofanyika chuo kikuu cha Miami nchini Marekani.

Mawimbi ya bahari na kupwa na kujaa kwa maji ya bahari kunasemwa kunachangiwa na mwezi, hasa wakati mwezi ukiwa mkubwa.

Tafiti zinaonyesha kuwa tabia za binadamu zimekuwa zikibadilika na kujirudia tena na tena kulingana na mzunguko na sehemu ambapo mwezi upo katika mzunguko wake.

Ukiachia mwezi,jua na nyota nyingine pia zimefahamika kuchangia mabadiliko haya ya tabia kwa binadamu.

[Soma pia:Alama za Nyota na Tabia za Watu:Tambua Misingi ya Tabia ZakoNyota na Kazi Zenye Mafanikio ]

Nafasi ya Mwezi na Mauji

Tafiti nyingi zilizofanya duniani zinaonyesha kuwa kipindi cha Mwezi-Mkuu(Mwezi unapokuwa juu na unaonekana wote) na kipindi cha Mwezi-Mchanga kunakuwa na mauaji mengi na kuwa mauaji hayo yamekuwa yakishuka kipindi cha mwezi unaposhuka na kuwa chini.

Katika kipindi cha mwezi mkuu na mwezi mchanga watu wengi wamefahamika kuchanganyikiwa zaidi kiakili kuliko kipindi kingine cha mwezi.

Wagonjwa wa akili na wenye magonjwa yanayohusu ubongo kama vile kifafa wamefahamika kuzidiwa zaidi katika kipindi hiki.

Uhalifu na ajali nyingi zimekuwa zikitokea sana wakati huu wa mwezi.

Mwezi-Mkuu na Kutokwa kwa Damu

Ukiachian uhalifu mwingi na magonjwa ya akili katika mwezi-mkuu,imefahamika pia kuwa watu hutokwa na damu zaidi katika kipindi hiki.

Upasuaji unaofanyika katika kipindi hiki ni hatari zaidi,na nyingi zimekuwa hazina mafanikio kwa sababu wagonjwa wanapoteza damu nyingi kipindi hiki.

Baadhi ya madaktari wamekuwa wakikataa kupanga upasuaji wakati wa mwezi mkuu na kusubiri wakati mwingine.

Kutungwa kwa Mimba na Jinsia ya Watoto Wanaozaliwa

Mzunguko wa mwezi umeonyesha kuchangia jinsia ya watoto wanaozaliwa.

Tafiti zimeonyesha kuwa mimba nyingi za watoto hutungwa wakati mwezi unapotoka gizani(mwezi mchanga kuelekea mwezi-mkuu) kuliko wakati mwezi unapoingia gizani(mwezi mkuu kuelekea mwezi-mchanga). Hii inamaanisha kuwa mimba zinatungwa kirahisi katika kipindi cha mwezi mchanga kuliko kipindi cha mwezi mkubwa.

Pia watoto wengi ambao mimba zao zilitungwa wakati wa mwezi unapotoka gizani ni wa jinsia ya kiume. Hivyo nafasi ya mwezi katika mzunguko inaweza ikasaidia wazazi kupanga jinsia ya mtoto watakao mzaa.

Mzunguko wa Mwezi na Mabadiliko ya Hisia za Wanawake

Wanawake wengi wamekuwa wakihisi mabadiliko ya hisia zao kulingana na mzunguko wa mwezi.

Mwezi unasemekana kuchangia mzunguko wa hedhi kwa wanawake. Mwezi huchukua siku 28 kukamilisha mzunguko sawa sawa na mzunguko wa hedhi kwa wanawake wengi.

Wanawake wengine huenda samabamba na siku za mwezi.

Inahisiwa kuwa kama mwezi una sababisha kupwa na kujaa kwa bahari,basi sababu hizo hizo za msukumo na mvuto wa mwezi na dunia ndio unaosababisha mabadiliko haya ya hisia kwa binadamu hasa wanawake.

Mwezi , Siku ya Kuzaliwa na Tabia za Watu

Tabia za binadamu zimegawanywa katika makundi kumi na mbili kulingana na sehemu mwezi na nyota nyingine ulipokuwa wakati wa kuzaliwa. Makundi haya yanaelezea tabia tofauti kwa watu waliozaliwa katika kipindi husika.

Makundi haya ni kama ifutavyo:

Mizani (Sept 23 – Okt22)
Nge (Okt 24- Nov 21)
Mshale (Nov 22- Des 21)
Mbuzi(Des 22 – Jan 19)
Ndoo (Jan 20 – Feb 18)
Samaki (Feb 19 – Machi20)
Kondoo (Machi 21 – Aprili19)
Ng’ombe (Aprili 20 – Mei21)
Mapacha (Mei 22 – Juni 20)
Kaa (Juni21 – Julai22)
Simba( Julai 23 – Agosti 22)
Mashuke(Agosti 23 – Sept 22)

Mwezi Mubwa na Kukosa Usingizi

Imefahamika kuwa watu wanaeleza kuwa na tatizo la kukosa usingizi wakati wa mwezi mkuu kuliko wakati mwingine.

Hivyo kuonesha kuwa mwezi unachangia mabadiliko hayo ya kitabia kwa maisha ya binadamu na dunia.

 

Ni kweli kuna madhara ya mwezi katika tabia na hisia zetu?

Japo tafiti na shuhuda toka kwa mtu mmoja mmoja zimetolewa, bado baadhi ya watu wanapingana na hoja hizi. Lakini wanapingana bila kuwa na ushahidi wa kitafiti hivyo hoja zao kukosa nguvu.

Bila shaka tafiti zaidi zitafanyika na kuleta makubaliano juu ya suala hili. Lakini sayansi ni juu ya kuona na kushuhudia, hivyo tunaweza kushuhudia wenyewe madhara haya ya mwezi katika maisha yetu kama tukifuatilia.

Fanya utafiti sasa na uone ukweli wake na unakaribishwa kuchangia unachojua katika sanduku la maoni hapa chini juu ya madhara ya mwezi katika tabia na hisia za binadamu ili tufaidike zaidi.

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment