Afya Zetu

Mambo 8 ya Kuharakisha Kuunga kwa Mifupa Iliyovunjika

Watu kwa mamia huvunjika miguu kote duniani kila siku kutokana na ajali mbalimbali hasa zinazohusisha usafiri kama magari na pikipiki. Wengine huvunjika wakiwa kazini na hata majumbani. Wote hawa wanahitaji kuunganishwa mifupa yao ili wapone na kuendelea na maisha.

Kuunga kwa mifupa iliyovunjika huchukua muda mrefu na hivyo kuwafanya watu waugue kwa kipindi kirefu na kushindwa kuendelea na kazi zao. Lakini kuna mbinu za kusaidia kuharakisha kuunga kwa mifupa iliyovunjika ambazo zikifuatwa zitasaidia watu kupona kwa haraka.

Kwa ujumla uungaji wa mifupa inategemea sana umri wa mgonjwa na ulaji wake wa chakula chenye virutubisho muhimu. Mchanganyiko sahihi wa madini,vitamini na protini ni jambo la msingi kuzingatiwa.

 Mambo 8 Muhimu Kuharakisha Kuunga kwa Mifupa Ilivyovunjika

 1. Madini ya Kalisiam (Calcium)

Kalsiam inachukua asilimia kubwa katika mfupa na ni madini muhimu sana katika kuunga kwa mifupa iliyovunjika. Kalsiam inapatikana katika vyakula lakini mgonjwa anaweza kutumia vidonge vyenye Kalsiam.

Ila ifahamike madini haya pekee hayatoshi,ni lazima kuwepo na vitu vingine kama vinavyoelezwa hapa chini

Vyakula Vyenye Kalsiam Kwa Wingi:

 • Mziwa na mtindi
 • Soya
 • Mboga za majani

 1. Vitamini Muhimu toka Katika Mlo Kamili

Mlo kamili wenye mchanganyiko wa vitamini,madini na virutubisho vingine muhimu katika mwili wa binadamu ni muhimu sana kwa mgonjwa aliyevunjika mifupa.

Vitamini D ,C na K zinahitajika kwa wingi kuharakisha kuunga kwa mifupa iliyovunjika.

Vitamini D:

Upungufu wa vitamini hii inafanya kalsiam isifike sehemu inayohitajika toka katika damu.

Vitamini D inasaidia kunyonywa kwa kalsiam toka katika damu na kuelekezwa katika mifupa iliyovunjika ili kusaidia uungaji.

Vyakula Vyenye Vitamini D kwa Wingi:

 • Samaki au mafuta ya samaki
 • Kiini cha mayai
 • Bidhaa za maziwa

Vitamini K:

Vitamini K inasaidia kuimarisha protini aina ya osteocalcin ambayo ni sehemu ya muundo wa mfupa. Vitamini K huifanya protini hii kuwa nzito na ngumu na hivyo kusaidia kuimarisha mfupa unaoounga.

Vyakula Vyenye Vitamini K kwa Wingi:

 • Mboga za majani
 • kauliflawa
 • Samaki
 • Mayai

Vitamini C:

Vitamini C inasaidia kupona kwa mifupa iliyovunjika. Vitamini C kama inavyosaidia kupona kwa vidonda inasaidia pia kuunga kwa mifupa kwa kusaidia kuundwa kwa chembe za kolageni (collagen) ambazo zinatengeneza mifupa.

Vyakula Vyenye Vitamini C kwa Wingi:

 • Machungwa na Ndimu
 • Kabichi na Mboga za kijani

 1. Kupunguza Matumizi ya Dawa za Maumivu

Dawa za kupunguza maumivu ni muhimu kwa mgonjwa aliyevunjika mifupa, kwani anakuwa kwatika maumivu makali hasa siku za mwanzo lakini dawa hizi pia zinasababisha kuchelewa kwa uungaji wa mifupa hivyo mgonjwa anashauriwa kutotumia kwa muda mrefu.

 1. Kuacha Uvutaji wa Sigara

Uvutaji wa sigara unachelewesha kupona kwa mifupa iliyovunjika. Wavutaji wa sigara wanashauriwa kusimama uvutaji wakiwa wagonjwa. Hii inachangiwa na sumu katika sigara kama benzini na karboni dioxide ambazo zinaingilia na kuharibu chembe za mfupa unaounga.

Lakini pia ni kwakuwa sigara inapunguza mzunguko wa damu mwilini kwa kufanya damu kuganda.

 1. Zuia Vyakula Vinavyonyonya Mifupa

Vyakula kama sukari,chumvi,pombe,kafeni na nyama nyekundu hufanya mifupa kulika kwa kupunguza madini ya kalsiam katika mifupa.

Vyakula hivivipunguzwe ilikuharakisha kuunga kwa mifupa iliyovunjika.

 1. Kuongeza Ulaji wa Kalori(Wanga)

Ilikuunga mifupa mwili unahitaji nguvu nyingi kufanikisha zoezi hili hivyo mgonjwa anashauriwa kula vyakula vyenye kuongeza nguvu. Inakadiriwa kiasi cha kalori 6,000 zinahitajika kila siku kwa mfupa uliothirika sana.

Mahitaji ya kawaida kwa mwanaume ni kalori  2500 na mwanamke wa umbo sawa ni kalori  2,000 tu.

 1. Ulaji wa Protini kwa Wingi

Mfupa unajengwa na protini hivyo inahitajika kwa wingi ili kujenga mfupa imara.


 1. Kufanya Mazoezi

Ili mifupa iunge kwa urahisi na haraka inahitaji mzunguko mzuri wa damu mwilini.

Kwa mgonjwa aliyevunjika hasa miguu huenda hili lisiwe jambo rahisi,lakini mazoezi yanaweza yakahusisha viungo ambavyo havijapata madhara ili mradi visaidie kufanya damu izunguke vizuri.

Mgonjwa anaweza kutembea hata kama anatumia magongo,au kufanya mazoezi akiwa amekaa ili mradi mzunguko wa damu uongezeke.

Mwisho

Kama wewe ni mgonjwa au una mgonjwa aliyevunjika basi njia hizi zitasaidia kuunga kwa mifupa iliyovunjika kwa haraka na kumfanya mgonjwa aendelee na shughuli zake za kawaida.

Asante kwa kusoma mada hii na nakutakieni afya njema. Ukiwa na mawazo maoni au maswali shiriki nasi kwa kuandika katika kisnduku hapa chini.

Sambaza “Upendo” washirikishe unaowapenda na kuwajali,bonyeza SHARE hapo ch

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment