Fedha na Uchumi Jamii Mafanikio

Mambo Ambayo Matajiri na Masikini Wanafanya Tofauti

Tajiri_Masikini

Kuwa tajiri au masikini inachangiwa zaidi na jinsi ya kufikiri na kutenda kuliko kitu kingine. Vitu hivi pekee ndivyo vinavyo watofautisha wale wanaofanikiwa na wasiofanikiwa katika utajiri wa mali au fedha.

Matajiri na masikini wanafikiria nakutenda kwa namna tofauti sana.

Kutajirika ni sayansi,kwa maana kuwa kuna vitu ambavyo ukivifanya kwa namna fulani na vilevile utapata matokeo yale yale kila mara.

Wachunguzi wa masuala ya mafanikio wanasema kuna vitu ambavyo ukivifanya kama ambavyo waliofanikiwa wamefanya basi yeyote yule atapata matokeo yaleyale-MAFANIKIO.

Leo tutachukua utajiri wa mali au fedha kama mojawapo ya mafanikio kwa binadamu.

Sasa je ni mambo gani ambayo matajiri wanafanya ambayo yanawafanya wawe matajiri ambavyo masikini hawafanyi?

 

#1: Utunzaji Mzuri wa Afya

Matajiri huweka miili yao katika hali ya afya njema kuliko masikini. Hupanga chakula cha kula chenye manufaa kwa miili yao, na hufanya mazoezi mara kwa mara.

Masikini wengi hawafanyi hivyo. Wanakula ovyo bila kujali madhara ya wanachokula. Wengi wanakufa kwa magonjwa yanayosababishwa na staili ya maisha kama magonjwa ya moyo na kisukari.

 

#2: Huweka Malengo na Hukazana Kukamilisha Lengo Moja

Imesemwa kuwa kama huna malengo basi kokote utakakoenda ni sawa kwako.

Matajiri wengi huweka malengo ya kufanikisha jambo fulani na hufanya kazi kwa nguvu zao zote kutimiliza lengo hilo kikamilifu.

Masikini wengi hawana malengo maalumu na hata kama wanayo basi hubadili mara kwa mara.

 

#3: Hufanya Mazoezi Mara kwa Mara

Matajiri wanajua umuhimu wa afya njema katika kutimiliza malengo yao ,hivyo hufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara katika kufanikisha hilo.

Masikini wengi hawana mipango thabiti juu ya afya zao na mazoezi ya mara kwa mara sio mojawapo ya mambo katika mipango yao.

 

#4: Huependa Kusoma Vitabu vya Kujiendeleza

Matajiri wengi wanajifunza vitu vipya kila mara hivyo wanasoma vitabu wakiwa safarini au kusikiliza Vitabu–Sauti (Audio Boks) wanapokuwa wakisafiri kwenye usafiri wa jumuia au binafsi.

Wanafahamu umuhimu wa kujiendeleza kielimu na husoma angalau kwa dakika 30 kila siku

Masikini hawasomi vitabu vya kujiendeleza. Kama wanasoma basi ni magazeti ya udaku au vitu ambavyo havisaidii maendeleo binafsi.

 

#5: Utunzaji wa Orodha ya Mambo ya Kufanya Kila Siku (To-Do-List)

Matajiri hupanga mambo ya kufanya na huandika kila siku. Wataalamu wa mipango na fikra za binadamu wanasema “kama hakijaandikwa basi hakipo”.

Masikini hawana mipango madhubuti na huwa hawaandiki mara nyingi.

 

#6: Wazazi Matajiri Huwafundisha Watoto Wao Kusoma Vitabu

Matajiri wanafahamu umuhimu wa kusoma vitabu katika maisha ya mafanikio. Wenyewe husoma mara kwa mara na huwafundisha watoto kuweka tabia ya kusoma vitabu vya kujiendeleza. Sio vya hadithi.

Masikini wengi hili si jambo la msingi. Wenyewe hawasomi na wala hawawezi kuwafundisha watoto vitu wasivyovifanya.

 

#7: Wazazi Matajiri Huwafanya Watoto Wao Kufanya kazi ya Kujitolea

Mwandishi maarufu kitabu cha Rich Dad Poor Dad, Robert Kiyosaki anasema –“Work to LEARN not to EARNyaani fanya kazi kwa ajili ya kujifunza na sio kutegemea kupata kipato.

Matajiri wanafahamu maana ya hili hivyo huwashauri watoto wao kufanya kazi bila kutegemea malipo kwajili ya kujifunza. Sababu katika mazingira ya namna hii mtoto anapata nafasi ya kufanya kazi na watu wenye uzoefu mkubwa na hivyo kujifunza zaidi. Elimu wanayopata inawasaidia kufanya bisahara zao baadae.

Masikini wengi hufanya kazi ili wapate malipo. Wazo la kufanya kazi kwa kujitolea halipo katika mipango yao.

 

#8: Huandika Malengo Yao
Matajiri huweka malengo ya muda mfupi na muda mrefu na huweka katika maandishi.

Masikini wengi hawaandiki malengo yao

Kwa masikini hili si jambo la mipango na kama linatokea basi si kwa malengo ya mafanikio ya kibiashara wala binafsi.

 

#9: Huangalia TV kwa muda Mfupi na Vipindi Halisia.

Matajiri huangalia TV kwa muda mfupi sana,sababu kubwa ni kuwa hawana muda wa kupoteza. Kwao Muda ni Pesa. Kwa masikini mabo si hivyo. Masikini wanaangalia TV muda mrefu sana hivyo kupoteza muda wao bure.

Matajiri pia huangalia vipindi vyenye uhalisia katika maisha. Kama mienendo ya kiabiashara, au michezo inayoelezea uhalisia katika maisha.

Masikini huangalia vipindi vyenye mantiki ya kufikirika zaidi kama tamthilia za mapenzi au ujambazi n.k.

 

#10: Matajiri Hauamka Masaa 3 Kabla ya Kazi Kuanza

Matajiri hulala muda mfupi sana. Hulala kati ya masaa 3-6 kwa siku. Masikini hulala kati ya masaa 10-14 kwa siku.

Matajiri huamka mapema kabla ya kazi kuanza. Hupanga mambo muhimu ya kufanya na pia huanza kazi kabla ya wengine. Wengine hufanya mazoezi wakati huu.

Kwao muda ni kitu cha thamani sana na hupanga na kuutumia vizuri.

Kwa masikini kuamka asubuhi sana ni usumbufu mkubwa. Masikini wengi ni wavivu.

 

#11: Matajiri Hupenda Kazi Zao

Matajiri wengi huanzisha biashara au kufanya kazi wanazozipenda. Hivyo hufanya kwa nguvu na uwezo wao wote na kufanikiwa.

Masikini wengi wanafanya kazi tu ilimradi inamplipa mshahara. Mwisho wa siku hawafanyi kwa ubora unaotakikana.

 

#12: Matajiri wana Uthubutu

Matajiri wengi duniani wana makampuni yao binafsi. Japo imesemwa kuwa kampuni 1 tu kati ya 10 zinazoanzishwa hubaki hai baada ya miaka 5 toka zifunguliwe, bado matajiri wanaanzisha makampuni na wengi wanafanikiwa.

Masikini wengi hawawekezi kwenye biashara binafsi. Wanapenda kuajiriwa zaidi ambako kunauhakika wa kupata mshahara kila mwezi.

 

#13: Hufanya Mitandao na Watu Wengine
Matajiri hutengeneza mitandao na watu wengine na kuiendeleza.

Hupenda kukutana na watu wapya na kutengeneza mahusiano ya kibiashara nao.

 

Haya ni baadhi tu ya mambo mengi ambayo matajiri wanafanya tofauti na masikini.

Kama unayo mengine basi ongeza katika sanduku la maoni hapa chini.

Kama mafanikio yanaweza kupatikana kwa njia ya kisayansi,kwa maana kuwa ukifanya mambo kwa namna fulani kila mara utafanikiwa kama ambavyo wengine wamefanikiwa. Hii inamaanisha kuwa basi kuna nafasi kwa kila mmoja wetu kuwa tajiri kama tutabadili mitazamo ya maisha yetu na kuanza kufahamu na kufanya yale ambayo waliofanikiwa wanafanya.

 

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment