Mafanikio

Mambo ya Kujifunza Toka Kwa Steve Jobs

kujifunza -toka-kwa-steve-jobs-1

Steve Jobs ni mwanzilishi wa Kampuni ya Komputa yenye mafanikio makubwa ya Apple Inc. Yeye na rafiki yake Steve Wozniak walianzisha kampuni ya kutengeneza komputa ya Apple Komputa  1 April 1976 na kusajiriwa rasmi 3 Januari 1977 huko nchini Marekani Jobs akiwa na umri wa miaka 21 tu na Wozniak akiwa na miaka 26. Jobs alikuwa bianadamu wakipekee kabisa na mwenye kibaji katika nyanja mbalimbali toka uongozi na hata utendaji wa moja kwa moja. Kuna mengi ya kujifunza toka kwa steve jobs kwa kila mmoja wetu.

kujifunza -toka-kwa-steve-jobs_jobs _na_wozniak-1

Steve Jobs na Steve Wozniak-Waanzilishi wa Apple Kompyuta 1976

Jobs aliiongongoza Apple kwenye mafanikio makubwa hasa kwa uwezo wakemkubwa wa kiuongozi na ubunifu. Japo Jobs alionekana kuwa na tabia zisioridhisha na kutoelewana na watu katika miaka ya mwanzoni lakini baadae alifanikiwa sana na anachukuliwa kuwa miaongoni mwa viongozi na mfano mzuri katika kufikia mafanikio.

Jobs alifariki dunia mwaka 2011 kwa ugonjwa wa kansa. Leo hii Jobs anakumbukwa sana katika kazi zake na ubunifu katika teknologia mfano ni ipad ,iphone na ipod. Kuna mengi ambayo tunaweza kujifunza toka kwake na tunaangalia mambo kadhaa ya kuigwa katika maisha yake binafsi na kama kiongozi na mfanyakazi wa Apples Inc.

 

Mambo 7 ya Kujifunza toka Kwa Steve Jobs – Mwanzilishi na Mmiliki wa Apple Komputa

  1. Kuongoza kwa Vitendo

kujifunza -toka-kwa-steve-jobs_onesha-mfano-2

Jobs alikuwa mzuri sana katika kubuni teknologia na ku zitangaza lakini alikuwa mtendaji wa mojakwa moja katika kubuni na kutengeneza bidhaa katika kila hatua. Alikuwa kiongozi wa kiufundi na alishiriki katika kila hatua za uzalishaji katika Apples.

Mojawapo wa mradi mkubwa aliousimamia ni Komputa ya Macintosh. Yeye mwenyewe alishiriki katika kubuni na utengenezaji wake ikiwemo kuitangaza.

Jobs hakuwa anasubiria ripoti mwisho wa siku au wiki,alikuwa akienda katika kila benchi la mfanyakazi na kujua kinachoendelea pamoja na kujua changamoto na kushiriki kwa kutoa ushauri wake au maelekezo.

  1. Mwanamasoko na Mtangazaji wa Bidhaa-Mtazamo wa Mtumiaji

kujifunza -toka-kwa-steve-jobs_mwanamasoko-1

Jobs alikuwa ni mwanamasoko mzuri wa bidhaa za kampuni yake,alikuwa mtu maalumu ambaye anatumiwa kufungua bidhaa mpya ikitoka kabla ya kwenda kwa watumiaji. Mikutano yake ya ufunguzi wa bidhaa mpya imekuwa ikihudhuriwa na mamia ya watu. Unaweza ukaona baadhi ya mikutano hii katika mtandao wa youtube.

i. Ufunguzi wa iPhone 2007

 

ii. Ufunguzi wa iPad 2010

 

 iii. Ufunguzi wa iPod Touch 2010

Alikuwa anatumia yeye mwenyewe kwanza kuona kama ataipenda ndipo iende sokoni. Vinginevyo inarudishwa kiwandani kwa maboresho zaidi. Alisema “Ukitaka kuuza wazo,bidhaa au huduma,jiweke mwenyewe katika nafasi ya mtumiaji”

Alikuwa mtu anayependa vitu vizuri na vyemye ubora na kwa tabia hii bidhaa za Apple zimekuwa bora sana katika soko hadi leo hii ukilinganisha na washindani wake ambao wengi wanaiga toka kwao.         

  1. Uongozi Bora wa Timu: Ajiri na Kufukuza Kazi – “Ajiri Waliobora Tu “

kujifunza -toka-kwa-steve-jobs_kiongozi-wa-timu-2

Steve Jobs alikuwa anaamini kuwa anauwezo mkubwa yeye mwenyewe na alikuwa anaamini mambo makubwa yatafanywa na watu wenye mtazamo wa mbali wenye kupenda wanachokifanya na wenye vipaji.

Alikuwa mjengaji mzuri wa timu ya kazi. Aliamini ili kuendelea katika kampuni ni lazima na muhimu kuwa na timu thabiti. Alijiita Timu A na alikuwa na usemi unaoenda “Watu wa Timu A huajiri watu wa timu A,Watu wa timu B huajiri watu wa team C”. Kwa kuwa alijiona mwenyewe kama mtu wa timu A hivyo aliajiri watu wenye uwezo wa juu na kuwaweka katika timu yake. Alifukuza yeyote ambaye alionekana kutojiamini ,mvunjaji moyo kwa wenzake na asiyeenda sambamba na dira ya kampuni au idara anayofanyia kazi.

Maendeleo mengi katika sehemu ya kazi yanarudishwa nyuma kwa ugumu wa viongozi kutowawajibisha watu wasio na sifa na wasio na uwezo wa kupeleka kampuni mbele,kwa mtazamo wa Steve hawa ni vikwazo na ni muhimu kuondolewa mara moja kwa mustakabali mzuri wa kampuni.

  1. Mwona Mbali na Mbunifu

kujifunza -toka-kwa-steve-jobs_mwona-mbali-1

Kama kiongozi mbunifu alikuwa mwona mbali,na anaonekana toka mwanzoni mwa kazi yake wakati akianzisha kampuni pamoja na rafiki yake Woziniak. Steve alikuwa akisema kuwa “tutengeneze bidhaa rahisi kutumia na bora ambayo itabadilisha ulimwengu” na alifanya kazi kila siku katika kuhakikisha hilo linatimia. Leo hii Teknolojia toka Apple imebadilisha maisha yetu bidhaa zao za MacBook,iPad,iPhone na iPod zinadhihirisha hilo.

Siri kubwa ya mafanikio ya Apples and Steve ipo katika ubunifu. Jobs ni alikuwa mzuri sana katika ubunifu. Jicho la mtumiaji ambalo alikuwa nalo lilisaidia sana katika kufanikisha kazi za ubunifu. Karibu kila mwaka Apples wamekuwa wakitoa bidhaa mpya na inayopendwa na watu.

Ukiangalia sana utaona kuwa hakuna mabadiliko makubwa sana bali nyongeza au maboresho machache yanayotokana na bidhaa ya nyuma na hili ndilo jambo linalotakiwa leo katika makampuni mengine yakiwemo yetu nchini mwetu.

Uboreshaji wa vitu ambavyo tayari tunavyo. Idara za Maboresho na Ubunifu zinahitajika sana katika makambuni uyetu na biashara tunazofanya-Vitu vidogo ambavyo vinaleta mabadiliko makubwa.

Angalia tabia za watumiaji,na angalia nini unaweza kubadilisha katika huduma au bidhaa unayozalisha na kuuza ambayo italeta mabadiliko katika soko-Hii ni siri ya mafanikio ya biashara

  1. Jifunze toka kwa Wengine

kujifunza -toka-kwa-steve-jobs_kujifunza-2

Steve Jobs alifanya kazi katika makampuni ya HP na Atari yanayoshulika na teknologia kabla ya kuanzisha kampuni yake mwenyewe.

Akiwa mfanyakazi katika makampuni haya ambayo tayari yalikuwa yameendelea alijifunza mambo yaliyomwezesha kufanya vizuri alipofungua yake.

Mwalimu wangu wa ujasiriamali Robert Kiyosaki anasema “Fanya kazi kwajili ya kujifunza na sio kupata fedha” Ni vizuri kujifunza kwa waliotangulia kwa maana hiyo kuajiriwa kutakupa faida moja kubwa-itakujenga ufahamu wa jinzi bishara ilivyo na jinsi huduma na bidhaa zinavyozalishwa na kuuzwa.

Wahitimu wetu wa vyuo wa leo na wale wa zamani tulioajiriwa tunatakiwa kulifahamu hili pia-Tuajiriwe kwa ajili ya kujifunza tu kisha tukihitimu tuanzishe biashara zetu

  1. Mzungumzaji Mzuri na Mshawishi

kujifunza -toka-kwa-steve-jobs_mshawishi-3

Steve alikuwa mzungumzaji mkuu katika Apple,alikuwa mshawishi wa hali ya juu na mfunguaji wa bidhaa kwa watumiaji kila toleo akiwa Apple.

Steve alimshawishi Mkurugenzi wa Pepsi Cola John Sculley kujiunga na Kampuni yake na kufanikiwa lakini alikuwa mshawishi mzuri katika kuuza komputa yao ya kwanza Apple I lakini pia katika kuajiri wafanyakazi wazuri wengi wakiacha kazi sehemu nyingine akiwemo Rafiki yake Steve Waziniak ambaye aliacha kazi HP.

  1. Fanya Unachokipenda Ili Kufanikiwa

kujifunza -toka-kwa-steve-jobs_fanya-unachokipenda-1

Jobs alikuwa na mapenzi makubwa na teknolojia na hili lilimfanya mwenyewe kuwa mtumiaji wa kwanza. Kama hakuipenda bidhaa basi ilitakiwa kurekebishwa.

Hata katika usaili wa wafanyakazi na kuchagua timu ukiachia akili na ubunifu alikuwa anaangalia sana mapenzi yake katika bidhaa.

Kwasababu kunamsukumo mkubwa wa mafanikio zaidi wa kupata fedha unaokufanya uendelee kufanya unachokifanya kwa mapenzi ili kufikia mafanikio. Steve anasema “Kama unafanya kitu usichokipenda basi ukiache na endelea kutafuta unachokipenda mpaka ukipate”

[Soma:Namna ya Kubadili Unachopenda Kufanya Kuwa Biashara]

Kwa Ufupi..

Jobs alikuwa Kiongozi aliyefanikiwa sana,Mbunifu,Mzungumzaji mwenye kalama,mwenye mapenzi na kazi yake na aliyeamini katika kazi ya timu. Haya ni mambo ya kujifunza toka kwa Steve Jobs na ukiyatekeleza katika maisha yako bila shaka utafanikiwa kwa viwango vyako kama ambavyo Jobs alifaniki

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment