Michezo

Lionel Messi Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia 2014. Je Alistahili?

Lionel-Messi-na-tuzo-Mchezaji-Bora-wa-Kombe-la-Dunia-2014

Lionel Messi akiwa na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia 2014

Hatimaye kombe la dunia 2014 limeisha na bingwa amepatikana-Ujerumani, wengi walitegemea hilo kutokana na jinsi timu hiyo ilivyokuwa ikifanya vizuri.

Argentina na Messi wao wamekosa kombe,inasikitisha kwa Messi lakini ameambulia Mpira wa Dhahabu.

Lionel Messi amechaguliwa kuwa Mchezaji bora wa mashindano ya kombe la dunia 2014 na kupewa tuzo la mpira wa dhahabu.

Messi mwenye umri wa miaka 27 sasa huenda hii ilikuwa ni karata yake ya mwisho kuweza kupata kikombe cha dunia. Yamkini kama atakuwa katika nafasi nzuri katika mashindano yajayo 2018 yatakayofanyika Urusi.

Unaweza kumwona Messi alivyokuwa na simanzi baada ya mechi ya fainali kuisha.

Waargentina walitakiwa kumvisha hadhi ya Diego maradona kama angeleta kombe nyumbani. Sina hakika sasa kama bado wanafirkiri Messi anamfikia Maradona kisoka. Mchambuzi wa soka katika mechi ya fainali katika televisheni ya taifa ya Tanzania (TBC) alisema “Maradona atabaki kuwa Maradona na Messi ni Messi,ni makosa makubwa kuwafananisha”.

Je wewe unafikiriaje? Hebu toa maoni yako chini ya makala hii.

Lionel-Messi-Mchezaji-Bora-wa-Kombe-la-Dunia-2014

Messi Alistahili Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia 2014?

Lakini swali kubwa ni je Messi alistahili tuzo hiyo?  Tumeona wachezaji wengine wengi wazuri katika mashindano haya kama Arjen Robben, Neymar, James Rodriguez na Thomas Mueller. Je ukilinganisha uwezo ambao hawa wengine wameuonesha katika mashindano haya unafikiri Messi alistahili kuwa Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia 2014? Au ilikuwa ni kumfuta machozi tu.

Messi mwenyewe alionekana kutofurahia kupokea tuzo na ni vigumu kusema kuwa alikuwa mchezaji bora katika mashindano ya haya ya 2014.

Japo tunajua mchango wake kwa Argentina kufikia fainal, amekuwa mchezaji bora wa mechi (Man of the march) mara nne na amefunnga magoli 4 lakini nathubutu kusema Messi hakuwa katika kiwango kizuri kama ambavyo tunamwona katika klabu yake ya Barcelona. Inasemekana amekuwa akicheza kama majeruhi.

Kocha wa Argentina Alejandro Sabella amenukuliwa akisema kuwa Messi alistahili tuzo hiyo ya mchezaji bora wa kombe la dunia 2014 kwani amewawezesha kufika fainali. Bila shaka hiyo ni kweli kwa timu yake.

Messi alifanya vizuri katika hatua ya makundi, na kufunga mabao manne katika michezo mitatu dhidi ya Bosnia, Iran na Nigeria lakini nyota yake ilikufa,na hakuweza kupata goli hata moja katika mechi za mtoano dhidi ya Uswisi, Ubelgiji, Uholanzi na Ujerumani.

Sijaona Messi “akikata msitu” yaani ile kuingi kati ya walinzi wa timu pinzani kama kawaida yake.

Hebu toa maoni yako juu ya mchezaji bora ambaye unafikiri angestahili zaidi kuliko Messi,tuandikie hapo chini ya makala.

Mtangazaji wa televisheni ya taifa ya Tanzania(TBC) amenukuliwa akisema “Katika hali ya kushangaza Messi amepewa tuzo ya uchezaji bora”. Huo ni mtazamo wake.

Messi aliwashinda wenzake tisa ambao pamoja nao waliteuliwa kushindania tuzo hiyo ambao ni
Angel Di Maria (Argentina), Javier MascheranoMaria (Argentina), Mats HummelsMaria (Ujerumani), Toni Kroos (Ujerumani), Philipp Lahm (Ujerumani) ,Thomas Müller (Ujerumani),Neymar (Brazil),Arjen Robben (Uholanzi) na James Rodríguez(Colombia).

&

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment