Utamaduni

Mitindo na Maadili ya Mavazi ya Kiafrika

mavazi ya kiafrika

Katika dhama za mawe mpaka mwanzoni mwa karne ya 19 kabla ya kuja kwa wazungu waafrika walikuwa na utamaduni wao-mfumo wa jinsi ya kuishi ukijumuisha lugha,ibada na mavazi.

Teknologia katika karne hizi ilikuwa chini sana ukilinganisha za mabara mengine yaliyoendelea kama Ulaya na Amerika.

Hata hivyo,historia inatuonyesha kuwa wazee wetu walikuwa na ubunifu wahali ya juu wa kutumia mazingira yao kuweza kujitengenezea vitu mbali mbali zikiwemo dhana za kilimo ,uwindaji,uvuvi,kupikia na hata utengenezaji wa mavazi yao.  Hata katika uchanga huu wa teknolojia waafrika waliweza kujitengenezea mavazi ya kuweza kujisitili-mavazi ya kiafrika.

Soma Pia: Mitindo Maridadi ya Nywele Asilia za Wanawake wa Kiafrika

Mavazi ya Waafrika Kabla ya Uvamizi wa Wageni

Inaaminika kuwa kabla ya biashara ya utumwa Afrika na Ulaya walikuwa na ukuaji sawa katika teknolojia,pengine inafikirika kuwa Afrika iliizidi Ulaya. Ugunduzi wa maandishi na ujenzi wa piramidi za Misri ni mojawapo ya ushahidi wa maendeleo haya ya Afrika.

Katika kipindi hiki waafrika walikuwa wakitengeneza mavazi yao na kujivika toka katika ngozi za wanyama waliokuwa wakiwawinda na magome ya miti ambayo yalilainishwa na kuwa kama nguo laini.

Walijivika maungo yao hasa sehemu za siri. Hii inaonyesha kuwa kuvaa kwa kuficha sehemu fulani muhimu mwilini ni utamaduni wa toka zama za mababu zetu. Hii inaweza ikaonekana hata leo katika baadhi ya makabila kama Wamasai.

Hata katika uhaba wao wa teknolojia waliweza kujitengenezea mavazi ya kusitili mwili.

Mavazi ya Waafrika Wakati na Baada ya Uvamizi wa Wageni

Wageni walipovamia Afrika kwa ajili ya biashara na kutafuta malighafi walikuja na tamaduni zao mpya zikiwemo za mavazi.

Waarabu na Wazungu walikuwa wameendelea  zaidi kiteknolojia katika karne hii na walihitaji malighafi kwa ajili ya viwanda vyao vya nguo huko kwao na Afrika kulikuwa ni sehemu muafaka kwa hilo.

Kwa kuwa nguo zao zilitengenezwa na mashine za hali ya juu kuliko zile za Afrika,Waafrika wakaanza kuvaa nguo za nje zaidi kuliko za kwao. Hapa ndipo kutawaliwa kwa mavazi kulipoanzia.

Walileta nguo na urembo mwingine na sisi tuliwapa ardhi na madini yetu. Na mbaya zaidi tuliwauzia watu wetu wenye nguvu na akili kama watumwa. Historia inasema asilimia kama 20% ya nguvu kazi ya Waafrika ilipelekwa utumwani.

mavazi ya kiafrika_karne-ya-19-mama-na-mtoto

Vazi la Mama wa Kiafrika na Mtoto Nyakati za Uvamizi wa Wazungu

mavazi ya kiafrika-karne-ya-19

Aina ya Vazi na Urembo wa Mwanamke wa Kiafrika katika Karne ya 19

mavazi ya kiafrika

Vazi la Wanawake katika Siku Maalumu

mavazi ya kiafrika_chifu

Vazi la Kiongozi wa Kiafrika-Chifu

Athari za Wazungu Katika Mavazi ya Waafrika

Wazungu walizibagua sana tamaduni za kiafrika na kuziita za kishenzi,na kupenyeza tamaduni za kwao yakiwemo mavazi.

Waafrika wakaanza kuvaa suruali na suti za kizungu. Wanawake nao wakaanza kuvaa suruali,hii pia nia athari ya Wazungu.  Kwa kuwa Wazungu waliwafanya Waafrika wafikiri kuwa kila kitu cha kwao ni kizuri namna ya uvaaji wa wafrika na maadili ya mavazi yao yakaanza kufifia.

Leo hii mavazi ya kiafrika yanavaliwa katika matukio maalumu tu na sio katika maisha ya kila siku ya nyumbani ama ofisini. Tunavaa  mavazi ya asili katika sherehe za harusi au za kuwaaga wali.

Baadhi ya mavazi leo yanaenda kinyume na maadili ya kiafrika. Kama tulivyoona hapo mwanzo kuwa wazee wetu katika umasikini wao wa teknolojia waliweza kuvaa mavazi kwa nia ya ufunika maungo yao,lakini leo hii ukiachia mendeleo makubwa katika teknolojia ya utengenezaji mavazi ,watu wanavaa mavazi yasiyo na staha yenye kuacha miili yao nje. Mavazi haya hayaendani na asili ya waafrika.

 

Mitindo ya Mavazi ya Kiafrika

Kuna mitindo mingi tu ya asili ya Afrika ambayo ni mizuri nayenye staha. Mavazi haya yanapendwa hata na wazungu wenyewe ambao tunafikiri kila kitu chao ni kizuri.

Hii hapa ni baadhi ya mitindo lukuki ya kisasa ambayo ina asili ya afrika na inavutia. Mingi ni ya kike kwani wanawake ndio wenye aina nyingi za mavazi.

a) Mitindo ya Wanawake

mavazi-ya-kiafrika_blauzi mavazi-ya-kiafrika_dela-1 mavazi-ya-kiafrika_gauni-2
mavazi-ya-kiafrika_gauni-5 mavazi-ya-kiafrika_kaptula mavazi-ya-kiafrika_suruali-1

b) Mitindo ya Wanaume

mavazi ya kiafrika mavazi ya kiafrika mavazi ya kiafrika
mavazi ya kiafrika mavazi ya kiafrika_shati-3 mavazi ya kiafrika

Ni wakati sasa waafrika waurudie utamaduni wao kwani Afrika kuna vitu vingi vizuri yakiwemo mavazi. Tuutunze na kuuenzi utamaduni wetu kwani ni mzuri na wenye maadili.

Mavazi ya kiafrika ni mojawapo ya vitu vingi ambavyo vina thamani kubwa na vinatufanya tujivunie uasili wetu-Uaf

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment

2 Comments