Jamii Utamaduni

Mitindo ya Kusuka Nywele za Asili:Jinsi ya Kuchagua Mtindo Bora

mitindo ya kusuka nywele

Wanawake wengi wa Kiafrika husuka nywele zao katika mitindo mbalimbali. Kwa wazungu na makabila mengine ambayo huwa na nywele nyingi na ndefu hupendelea kuchana zaidi.

Urembo wa kusuka nywele umekuwa wa aina mbali mbali. Aina nyingine ni rahisi kutengeneza na nyingine ni ngumu na zinahitaji muda mrefu kuzitengeneza nywele.

Mitindo rahisi kama vile kuchana na kubana huchukua muda usiozidi dakika 30 wakati mitindo migumu kama rasta ndogo na nyembamba zinaweza kuchukua masaa 10-20 kwa msusi mmoja.

Bei ya usukaji pia zinatofautiana kulingana na ugumu wa mtindo na muda unaotumika kusuka.

Mitindo ya Kusuka Nywele za Asili Isiyo na Madhara-Weavings na Relaxers ni Mbaya

Hapa tunapendekeza mitindo iliyo salama kwa taswira ya mtu-yaani isiyodhalilisha utu wako na ambayo haina madhara kwako kiafya.

Mitindo kama ya weaving inanyonyoa nywele na kuwafanya wanawake wabaki na vipara. Uwekaji wa madawa katika nywele kunakufanya uwe katika hartari ya magomnywa ya ngozi na saratani.

Mitindo hii pia inadhalilisha utu wa mwafrika kwani inaiga nywele za wazungu.

[Soma:Mitindo Maridadi ya Nywele Asilia za Wanawake wa Kiafrika ]

Mitindo Rahisi na Nafuu ya Kutengeneza Nywele:

1. Kunyoa Kipara:

Unaweza ukasema kuwa huu sio mtindo wa nywele,lakini ki ukweli ni mtindo maridadi kabisa na wanawake wengi wanautumia na wanapendeza.

Angalia baadhi ya warembo hawa wakiwa katika mtindo wa kipara

mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_kipara-3 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_kipara-2

2. Nywele Fupi za Kuchana au Kusuka:

Huu ni mtindo rahisi ambao unaweza kufanya mwenyewe nyumbani na ni wa haraka na hauhitaji pesa.

Kitana na kioo vinatosha.

 mitindo ya kusuka nywele-nywele fupi  mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_nywele_fupi-7  mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_nywele_fupi-3
 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_nywele_fupi-6    mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_nywele_fupi-5

3. Nywele Ndefu za Kubana:

Mtindo ungine rahisi ni kuchana na kubana katika namna tofauti. Unaweza ukatumia vibanio vya nywele au ukazifunga kwa kitambaa.

Mtindo huu ni rahisi na unaweza ukafanya mwenyewe. Unaweza kutumia mtindo huu katikati ya mitindo inayofunga nywele kama rasta na yeboyebo.

Nywele zinatakiwa kupumzika kidogo baada ya kusukwa katika mitindo ya kubana sana.

mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_kubana-1 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_kubana-2 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_kubana-3

Mitindo Migumu na Ghari ya Kutengeneza Nywele:

Mitindo hii ni migumu ,huchukua muda mrefu na hivyo ina bei za juu kusuka.

Msusi anashauriwa kutokaa sana na mitindo hii ya nywele,kwa afya njema isizidi miezi 2. Huduma kwaajili ya nywele pia ni muhimu kama kuweka mafuta na dawa za kuua wadudu kama mmba.

1. Rasta za Bandia:

Mtindo huu hutumia nywele bandia kusuka na ni nzuri na hupendezesha wanawake wengi.

mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_rasta-3 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_rasta-2

2. Rasta za Asili:

Hizi hazitumii nywele za nyongeza. Nywele asili husokotwa katika mafungu madogo madogo.

Wanawake wengi wamekuwa wakisuka mtindo huu siku hizi na unapanda chati.

mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_rasta-asili-1 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_rasta-asili-3 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_rasta-asili-2

3. Yebo yebo:

Ni mtindo maarufu sana nchini Tanzania na unapendwa na wanawake wengi. Umekuwa katika soko muda mrefu na bado unasukwa kwa wingi.

mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_nywele_yebo-yebo-3 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_nywele_ndefu-5 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_nywele_yebo-yebo-1

Mitindo Mingine ya Nywele:

Kuna mitindo mingine mingi na inayobadilika kila siku kulingana na wakati

Angalie aina nyingine hapa:

mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_rasta-1

Mitindo ya Kusuka Nywele ya Watoto:

Kwa kuwa mitindo hii ni salama kwa afya inaweza kutumika kwa watoto pia. Shule nyingi za Tanzania zinataka watoto wawe na nywele ndogo au wasuke mitindo rahisi.

Mitindo hii hapa inaweza ikawafaa watoto wako:

mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_watoto-4 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_watoto-3 mitindo-ya-kisasa-ya-kusuka-nywele_watoto-6

Chagua Mtindo Utakaokufaa

Kama ulivyoona kuna mitindo mingi ya kusuka nywele ,mingine ni rahisi na inahitaji muda mfupi wakati mingine ni migumu ,inahitaji muda mrefu na ni ya gharama kubwa.

Ukiwa na muda mfupi wa kujiandaa utahitaji mtindo rahisi,pia mtindo utakaouchagua utategemea tukio husika. Mtindo wa ofisini au safarini unaweza ukatofautiana na ule wa kwenye sherehe au shughuli nyingine ya kijamii.

Kumbuka mitindo ya kusuka nywele asilia ni bora na ni mizuri kwa afya yako ya mwili na kwa taswira yako kama mwafrika.

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment