Mafanikio

Namna ya Kuanza Mwaka Mpya Kwa Fikra Mpya za Mafanikio

mwaka-mpya-2015

Mwaka mpya ni wakati ambao watu wengi hujihakiki malengo waliojiwekea kwa mwaka uliopita na kujua mafanikio waliyopata na kuangalia wapi hawakufanikiwa na sababu za kutofikia malengo. Mwaka mpya ni kipindi muafaka kwa mipango na fikra mpya.

Huu wakati ambao wengi hupanga malengo na makakati mipya kwa mipindi kingine cha miezi kumi na mbili(12). Wengine wanasema siku yoyote inaweza kuwa ni mwaka mpya na ukafanya haya yote,lakini kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka ni muafaka kwasababu mabo mengi yanaenda na kalenda ya mwaka. Mifumo ya elimu,mabenki n.k hufuata miezi ya kalenda pengine hsa ndio maana mwanzoni mwa mwaka ni kipindi sahihi kuweka malengo binafsi na ya familia pamoja na mikakati ya utekelezaji wake.

Japo inasemekana malengo mengi hayafanikiwi kwa asilimia 60 lakini wale wanaoweka malengo wana nafasi kubwa zaidi ya kutekeleza kuliko wale wasiofanya hivyo.

Mwanzoni Mwa Mwaka ni Kipindi Sahihi kwa Fikra Mpya

Kama unataka kufanya mambo tofauti na ulivyokuwa ukifanya,na unataka kubadilisha matokeo ya mambo uliokuwa ukifanya kwa kipindi cha nyuma basi mwanzoni mwa mwakani kipindi sahihi. Fikiri tofauti na andika fikra zako ili uweze kufuatilia na kutekeleza kwa urahisi.

 Mambo 3 Makubwa ya Kuzingatia:

1.Kupanga Malengo

Andika nini unataka kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mfano

 • Kununua nyumba ya kuishi
 • Kupata shahada ya pili
 • Kununua gari jipya
 • Kuanzisha biashara ya duka la vifaa vya ujenzi
 • Kununua ardhi

 2. Kuweka Mikakati ya Kufikia Malengo

Malengo bila vitendoni sawa na ndoto tu. Kwa kila lengo unalojiwekea unahitaji kuweka mikakati ya jinsi ya kufanya kufikia malengo hayo. Orodhesha hatua utakazochukua kila siku katika kufikia lengo.

Mfano:

Lengo: Kununu nyumba ya kuishi

Mikakati:

 • Kuweka akiba asilimia 50 ya mshahara katika akaunti maalumu ya nyumba
 • Kuanzisha biashara ya kununua na kuuza nafaka na kuweka faida katika akaunti maalumu ya nyumba
 • Kuweka asilimia 5 ya mshahara katika SACCOS ili kuweza kupata mkopo mwishoni mwa mwaka kwaajili ya kuchangia manunuzi ya nyumba

3. Kuhakiki Utekelezaji wa Mikakati

Hatua hii husahaulika sana katika mipango. Ilikujua kama utekelezaji wa mikakati unafanyika kama ilivyopangwa ni muhimu sana kufanya uhakiki kila baada ya muda fulani. Kila mwezi au kila baada ya miezi mitatu. Hili litasaidia kujua kama upo katika njia sahihi na unapiga hatua au la.

Pitia malengo yako kila mara kwa jinsi iwezekanavyo na tekeleza kwa kufanya kwa vitendo kila siku kama ilivyopangwa.

Mambo Muhimu ya Kupanga Kufanya katika Mwaka Mpya:

 • Kubadili Tabia

Kama ulitaka kuacha kuvuta sigara au kubadiri tabia mbaya usiyoipenda basi hiki ni kipindi cha kufanya maamuzi haya magumu na ya msingi. Ni wakati ambao mwili uko tayari kupokea mabadiliko.

 • Kujiendeleza Kielimu na Kujifunza Kitu Kipya

Kama ulipanga kurudi shuleni tena na kuongeza elimu basi panga na ujiandikishe katika shule husika.

 • Kuanzisha Biashara Mpya

Kama unatamani kuwa mjasiriamali na kujiari mwenyewe au kuanzisha biashara ya muda wa ziada. Mwaka mpya ni kipindi sahihi kuanza. Andika mpango wako wa biashara,pata sehemu sahii ya biashara yako na anza mara moja hata kama una mtaji mdogo.

 • Pangilia muda wako Vizuri

Tenganisha muda wa kazi na familia. Gawa muda kwa kila jambo,muda wa kuwa ofisini kama umeajiriwa,nmuda wa kazi zako binafsi na kujiendeleza,muda wa kusoma,kufanya mazoezi,kusoma na kuwa na familia yako.

Andika ratiba utakayoifuata kwa kipindi kizima cha mwaka.

 • Panga Kununua Kitu cha Thamani

Unataka kujenga nyumba? Kama unayo tayari labda unataka nyingine kwaajili ya biashara. Panga namna ya kuweka fedha na kununua kiwanja au ardhi na kuanza ujenzi. Kama huwezi kununua ardhi na kujenga kwa kipindi cha mwaka mmoja basi unaweza ukapanga kwa hatua ambazo zinaweza kutekelezeka kwa wamu.

Pia unaweza ukapanga kunua gari au nyumba mpya. Andika wapi utapata fedha na mikakati ya kufanya kila siku kufikia malengo hayo.

Unaweza ;ia kupanga manunuzi ya vitu vingine kama kompyuta,mashine ya kilimo au mashine za kusaga nafaka.

 • Kulipa Madeni

Kama umekuwa ukidaiwa na unataka kuwa huru na madeni basi ni wakati wa kupanga namna ya kulipa na kuanza mara moja. Amua kuishi bila madeni. Amua kuishi kwa kipato chako na uwe huru.

 • Anza Kuweka Akiba ya Tahadhari

Kuna mambo yanayokuja bia taarifa. Magonjwa,misiba na dharura nyingine ambazo zinahitaji fedha. Ni vyema kuweka fedha kidogo kwa ajili ya kukabiliana nayo yanapotokea. Watu walio wengi hawaweki fedha za tahadhari kwani maisha yao ni mdomoni-kwenda-mdomoni,yaani wanachokipata chote kinatumika bila kuacha ziada.

Anza kuweka kiasi kidogo cha asilimia 1-10 kwa kila fedha unazopata. Anzisha akaunti benki kwaajili hii pekee. Weka fedha nyingine katika akaunti tofauti.

 • Anzisha Marafiki Wapya Wazuri

Mafanikio yako au kushindwa kwako ,munategemea sana marafiki ulionao. Tunafanya mambo mengi kulingana na ushawishi toka kwa watu tunaowaamini na kuwapenda hivyo nani anakuwa nawe muda mwingi kunachangia sana fikra zako na matendo yako.

Tengeneza marafiki wapya wenye tabioa njema na wenye mafanikio na utaona mafanikio mwishoni wa mwaka.

Jua ulikotoka na Panga Unakoenda

Ili kupanga na kufanikiwa katika mipango yako mipya kwa mwaka mpya ni muhimu sana kujua ulichopanga na kufanya kwa mwaka uliopita. Udhaifu wako unatakiwa kufahamika na kuufanyia kazi.

Nguvu zako zilizokufanya kufanikiwa mwanzoni zipanguiliwe vyema katika mwaka ujao ilikuleta mafanikio zaidi.

Je umeandika malengo yako na mikakati ya utekelezaji? Kama Bado fanya hivyo mara moja.  Kumbuka “Kama huna malengo kokote utakako kwenda ni sawa”.

&nb

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment