Biashara na Ujasiriamali Fedha na Uchumi

Namna ya Kuanzisha na Kukuza Biashara Kutumia Fedha Za Watu Wengine

kuanzisha-na-kukuza-biashara

Kupata fedha za mtaji wa kuanzisha biashara na kukuza biashara ni changamoto kubwa kwa wengi. Watu wengi tu wana mawazo mazuri ya biashara lakini wana kwamishwa na ugumu wa kupata mitaji ya fedha za kuanzia au kuendeleza biashara zilizokwishaanza.

Lakini wakati baadhi ya watu wakihangaika na fedha za mitaji wengine wanaweka benki mamilioni ya fedha ambazo hazifanyi kazi. Zinasubiria riba ndogo sana ambaayo ni sawa na hakuna. Makundi haya mawili kama yangekutana na kupanga mikakati basi kila upande ungeweza kufaidika.

Wenye mawazo ya biashara wangepeta fedha na kuweza kuzalisha faida ambayo ingeweza kulipa deni la mkopo na faida kukuza biashara na wakati huohuo waliotoa mkopo wa fedha wataweza kurudishiwa fedha ikiwa na riba kubwa kuliko ya benki.

Watu maridadi katika biashara na waliofanikiwa wanatumia mbinu hii kujenga biashara zenye mafanikio na kujijengea utajiri mkubwa. Wanatumia fedha za watu wengine kujitajirisha.

Zifuatazo ni mbinu 5 ambazo unaweza kuzitumia kupata fedha za kuanzisha biashara au kukuza biashara uliyonayo toka kwa watu wengine

Mbinu 5 za Kupata Fedha za Watu Wengine za Kuanzisha na Kukuza Biashara:

  1. Kukopa toka Benki au Mashirika ya Mikopo

kuanzisha-na-kukuza-biashara-mkopo-wa-benki

Benki ni sehemu moja kubwa kabisa ambayo unaweza kuitumia kuipata fedha za mtaji. Watu wenye fedha wanaweka fedha zao hapo kwa ajili ya usalama. Benki wanatumia fedha hizo kuzalisha zaidi kwakuwekeza katika sehemu mbalimbali ikiwemo kutoa mikopo kwa biashara zenye uwezo wa kurudisha kwa faida.

Unachotakiwa kuwaonesha benki ni kuwa unabishara yenye mpango mzuri na unaweza kurudisha fedha hiyo ikiwemo riba ambayo ni faida yao.

Unaweza ukaanza na kiasi kidogo tu kama Milioni 1-5 na ukiweza kurudisha kama inavyotakikana basi unakuwa umejenga uaminifu na hivyo kuwa rahisi unapoomba kwa mara nyingine.

Ukiwa katika kikundi klwabaadhi ya mashrikaya fedha ni rahisi zaidi kupata mkopo kuliko ukiwa peke yako.Ukiwa na mali kama ardhi,nyumba au hata gari unaongeza uwezekano wa kuaminika na kupewa mkopo.

  1. Kukopa toka Kwa Ndugu na Marafiki

kuanzisha-na-kukuza-biashara-mkopo-wa-ndugu-2

Ndugu zako au marafiki ni mojawapo ya sehemu ya kupata mkopo. Mara nyingi mikopo ya watu hawa haina masharti magumu sana,japo ni hatari kama utashindwa kurudishakama ilivyopangwa kwani utahatarisha uhusiano wako nao.

Wakati mmoja katika familia ni masikini au anakosa mtaji wa bishara kuna ndugu mwingine anafedha isiyotumika kukua na kuleta faida (Fedha iliyolala). Tafuta jinsi ya kushawishi fedha hii itumike kujizalisha na mazao ya mtaji huo uwafaidishe wote,wewe mkopaji na mwenye fedha.

Uaminifu ni kitu cha msingi sana katika kufanikisha hili. Ukiwa mtu unayeaminika ni rahisi kwa ndugu na marafiki kukuamini na fedha zao. Uaminifu ni mtaji mkubwa katika mchezo wa fedha.

  1. Kuingia Ubia na Wenye Fedha

kuanzisha-na-kukuza-biashara-mshiriki-1

Baadhi ya watu wenye fedha inawawia vigumu kuwaamini watu na fedha zao. Hawa unaweza kuwashirikisha katika utendaji na usimamizi wa biashara husika. Uza wazo lakokwao na uwashawishi waeke fedha. Kwakuwa wewe hauna fedha mchango wako utakuwa nguvu zako za kuendesha biashara hiyo (Mtendaji). Unaweza kumweka mshirika wako mwenyefedha katika maeneo ya kiuongozi hasa wa fedha ili alinde fedha zake na kujenga imani.

Njia hii ni rahisi zaidi kwani hauhitaji kulipa deni na ni rahisi mwenyefedha kuamini kwani yeye mwenyewe ni mshirika na anjua kinachofanyika.

  1. Vikundi vya Kuweka na Kukopa na Vikoba

kuanzisha-na-kukuza-biashara-vikundi

Vikundi vya kuweka na kukopa na vile vya kuchangiana kwa madhumuni ya kukusanya fedha nyingi ya kutosha kufanya jambo kubwa kwa mmoja wa wanakikundi ni jinsi mojawapo ya kutumia fedha za watu wengine kujiendeleza.

Tengeneza mpango wa biashara ambao una faida na chukua fedha katika kikundi chako ulichojisajili. Hakikisha bishara yako inaweza kurudisha fedha kwa wakati kulingana na masharti ya kikundi chenu.

  1. Pokea Malipo Kabla ya Kutoa Huduma

kuanzisha-na-kukuza-biashara-malipo-ya-awali-2

Ili kutengeneza bidhaa za kuuza,au kununua bidhaa ili uziuze unahitaji fedha kabla. Na hili linafanya wasio na mtaji kutoendelea na mipango yao.

Mbinu hii inakuhitaji wewe kutafuta mteja kwanza kabla ya kutengeneza au kununua bidhaa. Mteja akiwa tayari amekubali kununua atatakiwa kutoa malipo kabla,kisha unanunua bidhaa kwa fedha zake na kuwauzia kwa bei ya juu ili kupata faida. Kwa namna hii basi unakuwa unatumia fedha zao wenyewe kuendesha biashara yako na kutengeneza faida.

Wateja wanahitaji kukuamini sana ilikuweza kukupa fedha kabla ya huduma.

Benki si Sehemu Sahihi ya Kuweka Fedha

Benki ni sehemu ya kufanyia miamala na kuweka fedha kwa muda tu. Kama unahitaji fedha yako ikue na kukutajirisha ni muhimu kuitafutia sehemu ambayo itazalisha kwa haraka.

Kuwekeza katika biashara au mali zisizohamishika kama ardhi na majumba ni njia bora zaidi.

Kuwa mshirika katika biashara zenye mipango mizuri na zenye kuzalisha faida,nunua hisa katika makampuni na uwezekano wa kuzalisha fedha zako ni mkubwa kuliko kuweka benki.

 Elimu na Ujuzi wa Uongozi wa Bishara na Fedha ni Muhimu

Unahitaji kuwa na ujuzi na uzoefu wa kuendesha biashara na fedha ili uweze kupata fedha toka kwa watu. Wekeza katika elimu ya biashara,jisajili katika kozi ya uendeshaji biashara na fedha katika vyuo katika mji wako.

Pia soma vitabu vya kujiendeleza ili kukuza ufahamu wako.

Ukiwa na ufahamu mkubwa na ujuzi itakuwia rahisi kuaminika na hivyo kupata fedha toka kwa watu wengine.

Kuanzisha na kukuza biashara kwa fedha za watu wengine kumahitaji ushawishi wa hali ya juu ukiachia ujuzi na uzoefu uamininifu ni kitu kingine cha kuzingatiwa sana

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment

1 Comment