Biashara na Ujasiriamali

Namna ya Kubadili Unachopenda Kufanya Kuwa Biashara

kubadili-unachopenda-kufanya-kuwa-biashara

Inasemekana watu hufanikiwa sana katika kazi au bishara kama wanafanya kile wanachokipenda.

Na wataaluma wa ufanisi wa kazi wanashauri watu kutofanya kitu ambacho hawakipendi iwe kazi binafsi au ajira.

Sababu ni kuwa unapofanya kitu usichokipenda unakosa kuweka ubunifu na kwa kuwa unafanya bila moyo wako kuridhika huweki bidii za kutosha katika kazi hiyo. Matokeo ni wazi kuwa itakuwa mafanikio madogo.

Leo napenda kuzungumza jinsi ambavyo mtu unaweza kubadili unachopenda kufanya kuwa biashara. Unaweza kuchagua vitu ambavyo unavipenda na unafanya kwa ajiri ya mapenzi tu kuwa biashara itakayo kuingizia kipato.

1. Orodhesha Vitu Unavyopenda Kufanya:

kubadili-unachopenda-kufanya-kuwa-biashara_orodhaKwa kuanzia angalia vitu ambavyo unapenda kuvifanya katika maisha yako ya kawaida.

Viorodheshe katika karatasi, mfano inaweza ikawa unapenda kufanya manunuzi au kuangalia mitindo mipya ya mavazi madukani wakati wa mwisho wa juma.

Nyingine inaweza ikawa unapenda kuangalia tamthilia wakati wa jioni au unapenda Kuhudhuria sherehe na vikao vya maadalizi ya sherehe au vikao vya vikundi vya kijamii.

2. Angalia Kitu Kipi katika Orodha Kinaweza Kuuzika-Masoko:

kubadili-unachopenda-kufanya-kuwa-biashara_masokoKwenye kila kimoja katika orodha ,andika aina ya biashara itakayoanzishwa na angalia masoko yake. Yaani angalia kama watu wataweza wakakipenda na kununua.

Mfano:

  • Kama unatumia muda wa mwisho wa juma kuangalia mitindo mipya ya mavazi madukani na kufanya manunuzi basi andika jinsi ya kuanzisha duka la nguo litakalokuwa na aina ya nguo ambazo wewe mwenyewe unazipenda na kuziuza kwa watu wengine kama wewe.
  • Kama unatumia muda wa jioni kuangalia tamthilia na michezo ya kuigiza, basi andika jinsi ambavyo utaanzisha duka la kuuza diski za sinema na michezo ya kuigiza wakati wa jioni unapotoka kazini. Na katika kila tamthilia au mchezo utabandika muhutasari wa mchezo huo ili kumvutia mteja kabla hajanunua.

3. Chagua Biashara Moja na Andika Mpango Mradi(Business Plan):

kubadili-unachopenda-kufanya-kuwa-biashara_bplanKatika orodha yako chagua biashara moja ambayo unaipenda zaidi na inaonekana kuleta faida zaidi na iandikie Mpango Mradi. Ambapo utaelezea jinsi biashara hiyo itakavyofanyika,nani atafanya,kiasi cha fedha za awali utakazo hitaji,chanzo cha mtaji, bidhaa au huduma utakazotoa na bei utakazouzia kwa kila moja.

Mpango Mradi unakupa dira na mwelekeo wa biashara yako kabla hujaanza.

Wafanyabiashara wengi wanashindwa kwasababu hawaandiki Mpango Mradi.

Ukiwa na Mpango Mradi inakusaidia pia kupata mkopo toka katika taasisi za mikopo kama mabenki na SACCOS.

4.  Tengeneza Mpango-Masoko (Marketing Plan)

kubadili-unachopenda-kufanya-kuwa-biashara_mpango-masokoAndika jinsi ambavyo utaitangaza biashara yako ili watu waitue. Kama vile kutengeneza tovuti, kutengeneza na kusambaza kadi za biashara,vipeperushi na kutangaza katika vyombo vya habari kama redio,TV na magazezi.

Pia unaweza ukatangaza biashara kwa kwenda mtu mmoja mmoja au maofisini.

Unaweza pia ukafungua akaunti ya facebook kwaajili ya biashara yako na ukatangaza biashara

5. Fungua Akaunti ya Benki na Anzisha Vitabu vya Kumbukumbu za Bishara

kubadili-unachopenda-kufanya-kuwa-biashara_benkiMsemo maarufu unasema “Mali bila daftari hupotea bila habari” Kwa kuwa sasa hii ni biashara ni muhimu kutunza kumbukumbu za biashara kwa kuwa na vitabu kama risiti za mauzo,hati za madai (Invoice) na vinginevyo.

Pia ni muhimu kutunza fedha benki,hivyo utahitaji kufungua akaunti kwa jina la biashara.

Sasa biashara na wewe vimetengana. Fedha yako si ya biashara na ya biashara si yako mpaka taratibu maalumu zifuatwe kuweka au kuchukua fedha kwenda au kutoka katika bishara.

6. Jifunze Zaidi Kuhusu Biashara

kubadili-unachopenda-kufanya-kuwa-biashara_mafunzoUtahitaji kujifunza vitu mbalimbali kama vile uendeshaji bishara,kutunza mahesabu ya uhasibu,masuala ya kodi na kuongoza watu(wafanyakazi).

Unaweza ukajifunza mwenyewe kwa kununua vitabu na kujisomea au unaweza ukajiandikisha kwa kozi fupi katika chuo husika katika mji unaoishi.

Lakini njia nzuri kuliko zote ni kujifunza toka kwa watu wanaofanya tayari nawaliofanikiwa.

 

Kufanya kazi Masaa Yote

Kumbuka mwanzoni ulikuwa unafanya vitu hivi katika muda wa ziada labda baada ya kazi nyingine za mchana kutwa. Sasa kwa kuwa imeshakuwa biashara utahitaji kuipa muda zaidi ili iendelee kwa faida.

Mwanzoni unaweza kuajiri mtu wa kuifanya wakati ukiendelea na shughuli zako za kawaida na unaweza kuendelea kufanya mwenyewe baadae baada ya kazi za siku na wakati wa mwishoni mwa juma (Jumamosi na jumapili).

Baada ya biashara kufikia kiwango cha mapato ambacho kinaweza kukufanya umudu mahitaji yako ya kawaida na muhimu unaweza ukaacha kazi ya kutwa ya kuajiriwa na kufanya katika biashara yako binafsi kwa masaa yote.

Hebu anza leo kufanya haya,pata kipato kwa kufanya kazi unayoipenda badala ya kufanya bure na uongeze mapato katika familia.

Kama unahitaji msaada zaidi au una mawazo juu ya kubadili unachopenda kufanya kuwa biashara basi tuandikie katika kisanduku chini ya makala hii. Au tutumie barua pepe kupitia admin@bongoposts.com

 

&nb

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment