Sayansi na Teknolojia

Namna ya Kupata WhatsApp Katika Kompyuta

whatsapp-katika-komputa-0

Programu ya mawasiliano ya WhatsApp inayomilikiwa na FaceBook ambayo ina watu wapatao milioni 700 duniani kote sasa inaweza kupatikana kupitia kompyuta. Watumiaji hawa wanaweza kuweka na kutumia WhatsApp katika kompyuta.

Programu hii ambayo imekuwa ikiwekwa katika simu za smati (smartphone) sasa inaweza kupatikana kupitia brouza ya Google Chrome.

Mtumiaji wa Kompyuta atatakiwa kuweka brouza ya Google Chrome(Na sio nyingine yoyote) ili kuweza kutumia WhatsApp katika kompyuta. Hakuna program nyingine unayoiweka(install) au kuhitaji katika kompyuta yako.

Mahitaji ya Awali ili kuweza kuunganisha WhatsApp Katika Kompyuta:

Hakikisha yafuatayo kabla hujaanza zoezi hili:

  • Uwe na toleo la WhatsApp kwa Android kuanzia 2.11.498 na kuendelea. Hakikisha Simu yako ina toleo la mwisho la WhatsApp (Toleo la sasa tarehe 25/01/2015 ni 2.1.1.505)
  • Programu hii inafanya kazi katika simu zenye mifumo ya Android,Windows,BlackBerry,BlackBerry 10,na Nokia S60.
  • Brouza ya Google Chrome katika kompyuta unayotaka kutumia

Programu hii haifanyi kazi katika simu za iPhone na zile zinazotumia mfumo wa iOS za kampuni ya Apple.

Kuunganisha WhatsApp Katika Kompyuta

1. Utahitaji kwenda katika tovuti ya WhatsApp kutumia brouza ya Google Chrome na skani kutumia kamera ya simu yako picha nyeusi katika ukurasa huo

whatsapp-katika-komputa

2. Kwenye simu yako fungua menu katika WhatsApp na bofya WhatsApp Web

whatsapp-katika-komputa_menu

3. Simu yako itafungua kidirisha ambacho kitataka upige picha kisanduku hicho cheusi (unatakiwa kisanduku hicho kiwekwe katikati ya kidirisha chako katika simu,inaweza kukchukua muda kidogo kuweza kufanikiwa kutegemeana na simu na utulivu wako)

whatsapp-katika-komputa_skana

 

Ukifanikiwa basi simu yako na komputa vitakuwa vimeunganishwa.

Utaona taarifa zako za whatsapp kwenye simu katika komputa.

Kinachofanyika ni kuwa bado program yako ya whatsApp katika simu ndiyo inayotunza mawasiliano yote na ni lazima iweimeunganishwa wakati unatumia WhatsApp katika Kompyuta.

Maboresho na Changamoto:

Kama zilivyo program nyingine nyingi za simu au komputa tunategemea maboresho yafanyike katika program hii kama vile kuhakikisha mifumu mingine kama ya iphone na ipad iweze kutumika na whatapp ya webu. Lakini pia mlolongo wa kuunganisha kwa kupiga picha huenda ikawashinda wengi.

Binafsi nilichukua kama dakika 15 hivi kufanikisha. (Nilitakiwa kupunguza kidogo mwanga wa komputa ndio nikapatia)

Pia kudhibiti matumizi ya brouza moja tu (Google Chrome) itawafanya wengine wasiokuwa nayo na watakaoshindwa kuiweka kukosa huduma hii nzuri. Binafsi nimekuwa nikiihitaji sana kutumia Whatapp katika komputa.

Kuna brouza nyingine maarufu kama Internet Explorer,Mozilla Firefox,Safari n.k ,nafikiri itakuwa vyema kama Uongozi wa WhatApp watawezesha WhatsApp ya Webu ipatikane kwenye brouza hizo pia.

Faida za Kutumia WhatsApp katika Kompyuta

whatsapp-katika-komputa-2

Faida ya simu ni kuwa ni rahisi kushika na kubeba. Pia ni rahisi kwenda nayo popote-rahisi kubebeka. Lakini Kompyuta inakupa faida nyingine ambayo simu haina ambazo ni ukubwa wa skrini na urahisi wa kuandika kutumia kiibodi.

Hivyo katika mazingira ambayo mtumiaji wa WhatApp yanamwezesha kutumia kompyuta kama vile ofisini au nyumbani kama bila shaka komputa itakuwa chagua sahihi kwa kutumia WhatApp.

Asanteni kwa kusoma mada hii. Kama unapata tatizo kufuata njia nilizoelezea hapa basi usisite kuandika katika sanduku la maoni na kuomba masaada ili na wewe uweze kutumia whatsapp katika komputa.

 

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment