Matukio Nyinginezo Sanaa

“Nitampata Wapi”-Wimbo Mpya wa Diamond Platnumz

Msanii Maarufu wa Bongo Flava Diamond Platnumz ametoa wimbo wake mpya uitwao “Nitampata Wapi”. Unaweza kusikiliza na kuona video yake hapa.

Maswali ni kuwa je wimbo huu ameupiga maalumu kwa mpenzi wake waliyeachana hivi karibuni- Wema Sepetu? Au ulikuwa tayari katika mipango kabla ya hapo? Eti hata mwanamke anayecheza naye katika wimbo huu kafanana na Wema, sina hakika. Hebu angal;ia na toa maoni yako chini ya makala hii.

Kama ni “Nitampata Wapi” ni maalumu kwa ajili ya Wema Sepetu basi huenda wawili hawa wakarudiana tena siku za mbele,huwezi jua pengine sasa itakuwa milele na mile pamoja. Na pengine safari hii Diamond atakuwa na akili ya kiutu uzima kidogo na busara zaidi ya kuishi na mwanamke (mmoja).

Inasemwa kuwa “Mpenzi akitaka kwenda muache aende, akienda na akirudi tena kwako ujue ni wako milele”Toka katika Filamu “Indecent Proposal”

Japo baadhi ya washabiki wengine wanasema wimbo huu “Nitampata Wapi” ni wakawaida sana ukiachia video kuubeba, lakini wengine mimi nikiwemo naukubali na naona Diamond bado ni mmoja wapo ya wanamuziki wenye vipaji vikubwa sana ambao wamewahi kutokea Tanzania na Afrika Mashariki.

Kama akiweza kubadilisha tabia zake nje ya jukwaa na kujenga adabu kidogo kwa wapenzi wake basi ni wazi ni hazina kubwa kwa Tanzania katika tasnia ya muziki.

Najua mapokeo hasi ya baadhi ya wapenzi wake ni kwasababu ya tabia zisizoridhisha ambazo amekuwa akizionyesha mwanamuziki huyu na sio uzuri au ubaya wa muziki wenyewe. Ni somo kwa Diamond  kuwa nidhamu yake kwa watu na wapenzi ni muhimu sana katika kuendeleza kazi yake nzuri.

Toa mchango wako kuhusu winmbo huu na mwenendo wa Diamond kwa ujumla. Andika katika kisanduku cha maoni hapa chi

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment