Nukuu Muhimu

Nukuu Maarufu: “Mtu ambaye hajawahi kukosea hajawahi kujaribu chochote kipya”

Mtu-ambaye-hajawahi-kukosea-hajajaribu

 Wasifu:
Albert Einstein alizaliwa Ulm, Ujerumani Machi 14, 1879. Kama mtoto , Einstein alikuwa na udadisi ajabu juu ya kuelewa siri ya sayansi.

Alianza shule ya awali akiwa na umri wa miaka 5 katika shule ya Awali ya Wakatoliki.Alimaliza shule ya sekondari mwaka 1896.

Mwaka 1905 alipata shahada yake ya Udaktari(Ph. D) na kuchapisha makala zake nne za kitafiti zilizoleta ushawishi katika sayansi ikiwemo ile maarufu iitwayo“ Theory of Relativity” ambapo mkokotoo maarufu wa kifizikia wa “e = mc2 ulianzia.

Mwaka 1921 Einstain alipata Tuzo ya Nobeli

Einstein alihamia Marekani mwaka 1933 na akachukua makazi katika mji wa Princeton, New Jersey.

 

Hoja za Nukuu Maarufu:

Nukuu maarufu toka kwa Albert Einstein inahusu uthubutu.

Inasemekana , kama unataka kufanikiwa basi thubutu kujaribu kufanya kitu.

Utafiti unaonyesha kuwa watu wengi waliofanikiwa ni wale waliojaribu kufanya vitu ambavyo wengine wanogopa kufanya.

Makosa yanaweza yakawa ni kitu kizuri kama yataangaliwa kwa kutoka upande mwingine .
Kwa sababu katika kila kosa unalolifanya kuna nafasi ya kujifunza.

Katika njia ya mafanikio ni wazi kuwa kuna kuanguka, lakini kuanguka si kushindwa na hakutakiwi kuwa hivyo.

Simama, tathmini kwa nini umeanguka na ujifunze kwa makosa yako. Songa mbele.

Amini hutaanguka katika kikwazo kilekile tena hata kama utaanza upya kabisa.

 

Thubutu kuanza kufanya kitu kipya, kuthubutu kujitosa katika kitu ambacho hujawahifanya na MAFANIKIO yatakuwa ni MATOKEO y

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment