Nukuu Muhimu

Nukuu muhimu:”Sijashindwa,ila nimegundua njia 10,000 ambazo hazifanyi kazi.”

thomas-edison-kushindwa

Wasifu wa Thomas Edison:

Thomas Alva Edison alizaliwa tarehe 11 Februari 1847 na kufa tarehe 18 Oktoba, 1931.

Alikuwa Mvumbuzi wa Marekani na mfanyabiashara.

Ni mmoja wa watu maarufu na wavumbuzi wakuu, Thomas Alva Edison ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya maisha ya kisasa.

 

 Alitengeneza vifaa vingi ambavyo viliboresha maisha duniani kote, ikiwa ni pamoja na santuri, sinema, kamera, taa ya umeme na simu.

 

 Edison alikuwa mvumbuzi mkubwa na alipata hati miliki 1,093 za Marekani na nyingine nyingi Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani.

 Uvumbuzi wake umechangia sana katika mawasiliano ya umma na, hasa, mawasiliano ya simu.

 Mbali na kuwa mvumbuzi, Edison pia alikuwa mzalishaji bidhaa na mfanyabiashara.

 

Tafsiri ya Nukuu: Usikate tamaa hata kama unajaribu mara kadhaa na kushindwa.

 

Mazungumzo juu ya Nukuu:

Mafanikio yako yanategemea ni mara ngapi umejaribu. Kufanikiwa pia kunategemea pia mara ngapi umeshindwa na kujifunza kutokana na makosa yako.

Thomas Edison ni mvumbuzi ambaye amefamika kufanya majaribio mengi sana na mengi katika hayo yalishindwa,lakini hakuacha.  Aliendekea kujaribu mpaka pale alipofanikiwa.

Hivyo ukitaka kufanikisha jambo fulani katika maisha yako,basi thubutu kujaribu na hata kama utashindwa mara kadhaa,usikate tamaa jaribu tena na tena hatimaye utafanikiwa.

Katika kila jaribio unaloshindwa jifunze, ufahamu  nini kilikukwamisha ili mara nyingine unapojaribu usikwame katika kizingiti kile kile.

Vikwazo vyote vinapoisha kinachobaki ni mafanikio.

 

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment