Jamii Mafanikio

Nyota na Kazi Zenye Mafanikio

nyota

Kwa mujibu wa Wanajimu (Wanasayansi wa nyota) kila  mtu hapa duniani ana nyota yake katika mlolongo wa nyota kumi na mbili, kila nyota ina kazi zake za kufanya ili ufanikiwe zaidi katika maisha.

[ Soma PiaAlama za Nyota na Tabia za Watu:Tambua Misingi ya Tabia ZakoMadhara ya Mwezi Katika Hisia na Tabia za Binadamu:Kuna Ukweli? ]

 

Nyota ya punda(Aries).

ARIES-3D

Waliozaliwa tarehe 21 march- 19 april.

Kazi wanazotakiwa kuzifanya watu hawa ni jeshi, kazi za uokoaji, michezo, uuzaji, upasuaji, kufundisha(ualimu) na masuala ya fedha.

 

Nyota ya ng’ombe(Taurus).

Waliozaliwa tarehe 20 april- 20 may.

TAURUS-3D

Wenyenye nyota ya ng’ombe wanashauriwa kufanya kazi za muziki, kazi za chakula, ujenzi, kazi za mashamba, uhasibu na sanaa.

 

Nyota ya mapacha(Gemini).

Waliozaliwa tarehe 21 may- 21 june.

GEMINI-3D-300x266

Wenye nyota hii wanatakiwa kufanya kazi za utangazaji, uchapishaji, ualimu, ushari na biashara za kusafiri.

Nyota ya kaa(Cancer).

Waliozaliwa tarehe 22 june- 22 july.

CANCER-3D-300x202

Watu hawa wanatakiwa kujihusisha na kazi za madawa, kazi za baharini, upishi, kuhudumia watoto, kazi za benki, kazi za usimamizi na kazi za uandishi.

 

Nyota ya simba(Leo).

Waliozaliwa tarehe 23 july- 22 august

LEO-3D-300x227

Wenye nyota hii wanatakiwa kufanya kazi za usimamizi, michezo, usonara, uanamitindo, kucheza sinema, kazi za vijana na ualimu.

 

Nyota ya mashuke(Virgo).

Waliozaliwa tarehe 23 august- 22 september.

VIRGO-3D-285x300

Wenye nyota hii wanatakiwa kujishughulisha na uchapishaji, uongozi, elimu, afya, biashara na ukatibu mukhtasi.

 

Nyota ya mizani(libra).

Waliozaliwa tarehe 23 september – 23 october.

LIBRA-3D-300x210

Watu wa mizani wanatakiwa kufanya kazi za uhusiano wa jamii, ushauri wa ndoa, biashara yasanaa, ushauri wa mambo ya urembo, uanasheria na uhakimu.

 

Nyota ya ng’e(scorpio).

Watu waliozaliwa tarehe 24 october- 21 december.

SCORPIO-3D-300x284

Watu wa nyota hii wana takiwa kujihusisha na madawa, kazi za upelelezi, wachunguzi, mafundi bomba, kazi za historia ya mabaki ya viumbe na ushauri wa kimapenzi.

 

Nyota ya mshale(Saggitarius).

waliozaliwa tarehe 22 november -21 december.

dreamstime_9048880-300x288

Watu wa nyota hii wanatakiwa kufanya kazi za kusafiri,sheria, uandishi, ualimu, dini, michezo, jeshi na uuzaji.

 

Nyota ya mbuzi(Capricon).

Waliozaliwa tarehe 22 december- 19 january.

CAPRICORN-3D-300x230

Watu wa nyota ya mbuzi wanashauriwa kufanya kazi za uinjinia, uchoraji wa ramani za majumba, saveya , kazi za serikali, siasa na udaktari wa meno.

 

Nyota ya ndoo(Aquarius).

waliozaliwa tarehe 20 january- 18 february.

AQUARIUS-3D-241x300

Watu wa nyota hii wanatakiwa kujihusisha na kazi za ufundi wa umeme, kompyuta, uchunguzi wa kisayansi, kazi za kijamii, unajimu na kazi za mazingira.

 

Nyota ya samaki(Pisces).

waliozaliwa tarehe 19 february- 20 march.

PISCES-3D-270x300

Watu wa nyota ya samaki wanatakiwa kujihusisha na kazi za unesi, muziki, dansi, uigizaji, askari wa majini, kazi za kidini, kupiga chapa na kazi za kutoa ushauri.

 

Je unakubaliana na sayansi hii? Je ukiangalia maisha yako na ya wale unaowafahamu unaona ukweli juu ya uhusiano wa nyota na kazi?

Toa maoni yako hapa chini, bonyeza kwenye kisanduku cha “Comments”  kisha “Post Comments”

&

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment

1 Comment