Nukuu Muhimu

Nukuu Muhimu: “Omba Nguvu za Kukabili Maisha Magumu…”-Bruce Lee

Omba-Nguvu-Kukabili-Maisha-Magumu

Wasifu wa Bruce Lee:

Bruce Lee alikuwa ni Mmarekani wa asili ya Hong Kong. Alikuwa ni Msanii Mpiganaji,Muigizaji filamu za Kichina , Mwalimu wa kupigana,mtengenezaji wa filamu, na mwanzilishi wa mtindo wa kupigana wa Jeet Kune Do.

Lee alikuwa n mtoto mwimbaji nyota wa muziki wa opera Lee Hoi-Chuen.

Bruce anajulikana na wengi kuwa msanii maarufu zaidi katika fani ya upiganaji wa wakati wote

Lee alizaliwa Chinatown, San Francisco tarehe 27 Novemba 1940 na wazazi kutoka Hong Kong na alilelewa Kowloon na familia yake mpaka hadi alipokuwa kijana.

Aliingizwa katika fani ya filamu na baba yake na alionekana katika filamu kadhaa wakati huo kama muigizaji mtoto.

Lee alihamia Marekani akiwa na umri wa miaka 18 ili kupata elimu yake ya juu, katika Chuo Kikuu cha Washington, na ni wakati huu ndipo alianza kufundisha ujuzi wa kupigana.

Filamu zake nyingi alicheza Hong Kong na Holywood na kufanya filamu za kichina kupanda cati sana katika nchi za magahribi katika miaka ya 70.

Umahiri wake ulionekana sana katika filamu tano maarufu: The Big Boss (1971) na Fist of Fury (1972); Way of Dragon (1972), Enter the Dragon (1973) na Game of Death (1973)

Lee alikuwa na uraia wa nchi mbili, Hong Kong na Marekani.

Bruce Lee alikufa Kowloon Tong,Marekani Julai 20, 1973 akiwa na umri wa miaka 32.

 

Tafsiri ya Nukuu:

Omba msaada kujifunza mbinu na ujuzi wa kukuwezesha kupata mahitaji yako na sio kuomba mahitaji yenyewe bila kujua jinsi ya kutafuta na kukufanya kuwa mwombaji na tegemezi kila mara.

 

Mazungumzo Juu ya Nukuu:

Msemo huu unafanana na ule usemao “Ukitaka kumsaidia mtu,usimpe samaki,bali mfundishe kuvua samaki”.

Maombi yetu yawe ni kwa ajili ya kujenga mfumo na sio kuomba matokeo yaani kuommba vitu vilivyokamilika. Ukijenga mfumo unakuwa na uwezo wa kuutumia kuleta matokeo tofauti (Matunda ya mwisho);utaweza kutumia mfumo ambao unahusisha elimu,ujuzi na mbinu za kutengeneza matokeo unayotaka.

Unahitaji msaada mara moja tu kujenda mfumo, na utahitaji msaada mara mia moja kama utaomba matokeo au matunda ya mwisho.

Unapoomba kitu kilichokamilika unakosa kufahamu mbinu na ujuzi uliotumika katika kukitengeneza au kukipata kitu hicho. Hivyo kukufanya uwe tegemezi kila unapohitaji. Ukiomba mbinu na ujuzi unapata faida ya kutohitaji msaada kila mara unapohitaji badala yake utatumia ujuzi na mbinu kutafuta vitu ili kutimiliza mahitaji yako kila yapoto

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment