Michezo

Pele Aitisha Brazil Kwenye Ardhi Yao

peleGwiji wa soka duniani, Edson Arantes do Nascimento’Pele’, amewaambia Brazil waombe wasikutane na Hispania.

Pele ambaye amewahi kuipa Brazil mafanikio makubwa kipindi alipokua mchezaji, alisema”Hispania wanatimu nzuri sana hivyo wanatakiwa kuomba wasikutane noa kama wanataka kuchukua ubingwa wa dunia”.

Michuano ya kombe la dunia inatarajiwa kuanza kutimua vumbi juni 12 nchini Brazil na nchihizo zinategemewa kuongoza makundi yao.

Aidha pele alisema Hispania ni timu nzuri yenye uwezo wa kumiliki mipira katika mchezo, hali inayofanya wacheze vizuri, kama Brazil itataka kushinda kombe la dunia basi waombe wasikutane nao.

mwisho Pele alisema hata kama Brazil wanatimu nzuri lakini wanakosa vitu muhimu, huku akiongeza kuwa kama wangekuwa na mshambuliaji kama Diego Costa timu ingekuwa nzuri.

 

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment