Sayansi na Teknolojia

Programu 10 Muhimu za Simu za Android kwa Habari za Tanzania

programu-za-android-2

Simu za Android ni mapinduzi makubwa katika technolojia ya habari na mawasiliano. Simu hizi zinakuwezesha kuweka programu mbalimbali kadiri ya mahitaji yako. Kuna prohramu kama facebook,twitter,whatsapp kutaja chache tu.

[Soma Pia: Programu 30 za Simu ya Android Muhimu Kuwa Nazo]

Imesemwa kuwa “Taarifa ni Nguvu” yaani mtu mwenye taarifa nyingi na muhimu ni mwenye uwezo wa kufanya mengi au kushinda vingi. Ukiachia vyombo vingine vya habari vilivyozoeleka kama redio,TV na magazeti sasa hivi unaweza ukapata yote haya kupitia simu ya android. Kuna programu ambazo zinakuwezesha kusikiliza redio,kuangalia TV na kusoma magazeti. Chombo kingine cha habari kilichoongezeka ni intaneti. ambayo inakuwezesha sasa kupata habari kupitia tovuti,blogi na mitandao ya kijamii.

Hapa tutaangalia programu za habari za Tanzania ambazo zinaweza kuwekwa katika simu za android

 

# 1. Tanzania News, Radio & Video

Inakuwezesha kupata habari mbalimbali toka katika magazeti yanayoongoza Tanzania.

Habari toka katika vitu vya redio na Televisheni.

Inakuwezesha kupata habari popote,uwe ndani ya nchi au nje.

Unaweza pia kumtumia rafiki yako habari uliyopendezwa nayo moja kwa moja toka katika programu hii.

programu za-simu-ya-android_tanzania-newspapers-and-video

 

# 2. Tanzania Newspapers And News

Habari zinazovuma zaidi katika magazeti ya Tanzania

programu za-simu-ya-android_tanzania-newspapers-and-news

# 3. Tanzania Newspapers

Habari mbalimbali za magazeti ya Tanzania na ya nje pia.

Inapanga habari katika makundi kukuwezesha kusoma kirahisi.

Unaweza kusoma hata kama mtandao umekatika.

Unaweza kuwashirisha marafiki katika WhatsApp, Twitter, Facebook, Google+, SMS na barua pepe.

programu za-simu-ya-android_tanzania-newspapers-2

# 4. Tanzania Jobs

Habari juu ya nafasi za kazi nchini Tanzania.

Kama unatafuta kazi au unamtafutia kazi mtu programu hii itakusaidia kupata taarifa hizo kila mahali ulipo.

programu za-simu-ya-jobs-2

# 5. YellowPages Tanzania

Programu inayokupa taarifa toka Kitabu cha orodha za biashara cha Yellow Pages.

Kinaonyesha anuani na mawasiliano ya watu na kampuni mbalimbali nchini Tanzania

# 6. Tanzania Tanzania TVs

Inakupa vipindi vilivyorekodiwa toka katika TV mbalimbali Tanzania.

Orodha ya vipindi:

 1. ITV Tanzania
  2. EastAfrica TV
  3. Clouds TV
  4. Michuzi Blog
  5. Swahili Wood
  6. Chadema TV
  7. The Sporah Show
  8. Orijino Komedi
  9. Bongo Star Search
  10. Millard Ayo
  11. Mkasi TV
  12. Bongo 5
  13. Gonga MX
  14. Kansiime Anne and
  15. CNN International

programu za-simu-ya-android_tanzania-tv-1

# 7. Tanzania Radio Stations

Sikiliza radio mbalilmbali za nchini Tanzania toka katika simu yako kupitia programu hii.

programu za-simu-ya-android_tanzania-radio-stations

# 8. Tanzania Blogs

Mkusanyiko wa blogi maarufu nchini Tanzania.

programu za-simu-ya-android_tanzania-blogs

# 9. JamiiForums

Majadiliano ya kifikra toka mtandao maarufu wa Jamii Forums

programu za-simu-ya-android_jamiiforums-1

# 10. Tanzania Facts

Taarifa mbalimbali kuhusu tanzania. Mfano jiografia,serikali,uchumi,mawasiliano,usafiri n.k

programu za-simu-ya-facts

Namna ya kupata Programu Kwenye Simu

Bonyeza katika jina la programu au picha ili uweze kuweka programu husika katika simu yako.

Kumbuka kuwa programu hizi zinahitaji uwepo wa mtandao wa intaneti katika simu yako na gharama za matumizi zitachajiwa katika mfumo wa kawaida wa matumizi toka kwa mtandao husika.

Kama kuna progamu nyingine za habari za simu za android unazotumia na hazipo katika orodha yetu, basi tafadhari ziongeze katika kisanduku cha majibu hapa chini.

 

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment