Michezo

Rachel wa Bongo Movie kuagwa kesho

RachelHaule539

STAA  wa filamu za kibongo, Rachel Haule ‘Recho’ aliye fariki dunia juzi jumatatu anatarajiwa kuagwa kesho jijini Dar es salaam.

Marehemu alifariki dunia katika Hospitali ya muhimbili ambako alilazwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum baada ya kujifungua mtoto aliyefariki muda mfupi baadaye.

Taratibu za kuagwa na kusafirishwa kwa mwili wa marehemu, zinaendelea chini ya Mwenyekiti wa Bongo movie Steve Nyerere ilikuona jinsi ya kusafirisha mwili wa marehemu  kuelekea kwao Ruvuma.

Marehemu’Recho’ ameigiza kwenye filamu ya Figo na Mke mwema huku akijipatia umaarufu mkubwa katika tasnia ya filamu.

Msiba huu ni siku chache baada ya msiba wa mwigizaji na mwongozaji wa Bongo movie Adam Kuambiana.

Mungu amlaze mahala pema peponi -Amina.

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment