Jamii

Usawa wa Kijinsia Unacheleweshwa na Upendeleo Kwa Wanawake

usawa-wa-kijinsia

Usawa wa Kijinsia unahusu mtazamo kwamba wanaume na wanawake wanapaswa kupata nafasi na haki sawa, na haipaswi kubaguliwa kwa misingi ya jinsia, isipokuwa kama kuna sababu za kibiolojia.

Usawa wa kijinsia haimaanishi kwamba wanawake na wanaume ni sawa, lakini kwamba wana thamani sawa na ni lazima wapewe nafasi sawa kulingana na vigezo stahiki kama vile juhudi katika utendaji,taaluma na uzoefu.

Kampeni hizi zina historia ndefu na zimekuwa zikifanyika kote duniani ikiwemo Tanzania.

Umoja wa Mataifa (UN) uliweka azimio juu ya  Haki za Binadamu zikiwemo haki za wanawake kupata nafasi sawa na wanaume. UN inasema kuwa kuwawezesha wanawake pia ni chachu muhimu kwa ajili ya maendeleo na kupunguza umaskini.

Dhana hii imepewa mkazo sana nchini Tanzania na hata inapitiliza upande wa pili na kuwa wanawake pengine wanapata zaidi kuliko wanaume katika maeneo fulani na wanaume kukosa kwa sababu tu ya jinsia yao.

Kuwapa Wanawake Zaidi Kunaturudisha Katika Tatizo Lile Lile

Hoja ya leo inalenga juu ya kutoa nafasi sawa  kwa kuweka vigezo na mazingira sawa kijamii,kisiasa na kuuchumi ili wote, wanawake na wanaume waweze kushiriki katika harakati za kimaisha. Katika kutekeleza dhana hii huenda baadhi ya mambo yanapitiliza na wanawake wamekuwa wakipewa vitu zaidi kuliko wanaume na kurudi katika tatizo lile lile la awali la utofauti wa haki za kijinsia.

Nitaelezea maeneo kadhaa ambayo nafikiri yamepitiliza upande wa pili na yanahitaji kuangaliwa:

i. Uchaguzi wa nafasi za masomo katika taasisi za elimu toka sekondari hadi vyuoni:

Ili kuongeza nafasi zaidi kwa wanawake kumekuwa na mikakati ya kupendelea wanafunzi wakike zaidi. Kama mwanafunzi wa kiume amepata alama sawa na wa kike basi yule wa kike atachukuliwa na wakiume ataachwa. Kosa lake tu ni kuwa mwanaume. Hii haijengi usawa unaozungumziwa katika dhana ya awali.

Kumekuwa na Programu maalumu katika baadhi ya vyuo vya Tanzania ya kuchukua wanafunzi wa kike katika fani ya sayansi na kuwapa mafunzo ya awali ya ziada kabla ya kuchaguliwa kwa upendeleo kuingia katika kozi za sayansi. Wanafunzi wa kiume ambao wanapata alama sawa na hawa hawapati nafasi hii kwa sababu wamezaliwa wanaume.

Hili linawafanya wanawake waonekane kuwa ni watu wasiojiweza na wenye kuhitaji msaada. Hili linaongeza tatizo la jamii na hasa wanaume kuwaona wanawake kama viumbe dhaifu visivyojiweza na vinavyohitaji msaada ili kuendelea katika maisha.

ii. Nafasi za Uongozi na Uwakilishi wa Jamii

Nafasi za kuteuzi katika wizara na taasisi ka kuangalia jinsia sio tu kunapunguza ufanisi wa kutendaji kama anayepewa nafasi shana vigezo staiki bali pia kunatengeneza hali ya dharau kwani wanaonekana kuwa ni dhaifu tu na wanapata nafasi hizi kwa hisani tu.

Viongozi wanaoteuliwa au kuchaguliwa waendane na vigezo vya elimu na uzoefu na sio kuangalia kama ni mwanamke au mwanaume. Hili ndilo linaloelezea usawa wa kijinsia.

Kutoa nafasi za uongozi kwa mtazamo wa jinsia unawafanya wanawake wabezwe juu ya uwezo wao  na wanaume na kufanya usawa wa kijinsia kama kunavyoelezewa katika dhana yenyewe kupotoshwa.

Nchini Tanzania kuna viti maalumu kwa wanawake,kigezo cha viti hivi maalumu ni kuwa mwanamke. Kufanya hivi kunamnyima haki mtanzania mwingine mwanaume mwenye vigezo sawa.

iii. Kufanya Kazi Fulani katika Jamii:

Mkiwa safarini na gari likaharibika au kukwama. Utasikia kondaka akisema “Wanaume tushuke tusukume gari” na wanawake wanaogombea haki sawa wanakaa kimya na kupokea upendeleo wa aina hii.

Wanaume watashuka na kusukuma gari na pengine baadhi ya wanawake wakiwa bado ndani ya gari.

Mtazamo ni kuwa wnawake ni dhaifu au hawana nguvu za kufanya kazi kama hizi. Kama wanawake wana nia ya kweli ya kufikia usawa basi wakatae upendeleo unaopitiliza kama huu.

Katika kijiji nilichotoka na maeneo ya karibu kazi za shamba na nyumbani zimegawanyika katika makundi kadhaa  na baadhi ya makundi yanafanywa na watu wa jinsia fulani tu. Mfano, Ili kuandaa shamba jipwa ,miti hukatwa kwanza (Kwa Kingoni: “Matema“) hii ni kazi ngumu sana na wanaume pekee ndio wanaoifanya. Labda kwa sababu inaaminika kibayolojia wanaume wana nguvu zaidi. Lakini kwa mtazamo wangu aina hii ya ubaguzi haupelekei kufikia dhana ya haki sawa kijinsia,misemo kama hizi ni kazi za kike au za kiume zinatokana na mgawanyo huu wa kazi katika jamii yetu.

Tofauti kati ya Mwanamke na Mwanamme

# 1. IQ: Uwezo wa Kuchanganua Mambo-Hakuna utofauti mkubwa

Utafiti unaonesha kuwa hakuna utofauti mkubwa katika uwezo wa kuchanganua mambo kati ya mwanamke na mwanamme kupitia kipimo cha IQ.

# 2. Mfumo wa Ubongo na Fikra:

Matokeo ua kitafiti unaonesha utofauti mdogo kwa namna ambavyo wanawake na wanaume wana fikiri (how-mens-brains-are-wired-differently-than-women)

Ubondo wa mbele: Huongoza mambo ya vitendo(Action)
Ubongo wa nyuma: Huongoza mambo ya ufahamuna utambuzi (Perception)
Upande wa Kushoto: Huongoza fikra za uchambuzi wa kimantiki
Upande wa Kulia: Huongoza mambo yasiyohitaji kufikiria

 

usawa-wa-kijinsia

Mtiririko wa fikra katika ubongo wa mwanamme (Kushoto) na mwanamke(Kulia)

Wanaume wametambuliwa kufikiri zaidi katika uelekeo wa mbele na nyuma na kuwafanya waweze kujengeka kirahisi katika mambo yanayohitaji haraka na nguvu hasa za misuli.

Kwa upande mwingine wanawake wanauwezo mkubwa zaidi wa kufikiri katika uelekeo wa kushoto na kulia hivyo kuwafanya wawe na uwezo mkubwa kujengeka katika mambo yanayohusu kufikiria kwa kina na mambo yanayohitaji maammuzi yasiyo ya kifikra (Intuitive).

Wanaume ni wazuri katika mambo yanayohusu vitu wakati wanawake ni wazuri katikamambo yanayohusu watu.

Ushahidi huu unaweza ukawaongoza watawala na viongozi kuchagua watu katika nafasi fulani kulingana na jinsia.

Katika hali kama hii ni muhimu kuangalia vigezo hivi vya kibayolojia juu ya vile vya kitaaluma.

# 3. Muundo wa Mwili: Kuna Tofauti Chache

Urefu:
Wanaume na wanawake wanatofautiana ki muundo wa mwili. Wanaume kwa kawaida ni warefu kuriko wanawake. Wastani wa urefu wa mwanamke: 5’10” (Futi 5 na nchi 10) wakati kwa wanawake ni 5’4” (Futi 5 na nchi 4).

Kiasi cha mafuta mwilini: Wanawake 26% wanaume 13%

Uwezo wa Mapafu:
Wanawake wana mapafu madogo na yana nguvu ndogo kwa asilimia 30 chini ya mwanaume.

Mgawanyiko wa Misuli na Nguvu Mwilini:
Wanaume wanamisuli na nyama nyingi zaidi juu ya kiuno wakati wanawake wana nyama nyingi na misuli chini ya kiuno.
Wanaume wanahitaji kiasi kikubwa cha nguvu (kJ) mwilini kwa siku kuliko wanawake na wanaonekana kuwa na nguvu zaidi za kimwili kuliko wanawake (kwa asilimia 50 zaidi ya wanawake).

Wanawake wanachoka haraka zaidi kuliko wanaume kwa sababu damu ya wanawake ina maji zaidi na kiasi kidogo zaidi cha chembe nyekundu za damu chini kwa asilimia 20 ukilinganisha na wanaume.

Hii pengine ndiyo inayopelekea mgawanyiko fulani wa kazi katika jinsia. Kazi zinazohitaji nguvu zaidi zinafanywa na wanaume zaidi kuliko wanawake.

usawa-wa-kijinsia-muundo-wa-mwili-1

Kiujumla Hakuna tofauti kubwa kati ya Mwanamke na Mwanaume
Kwa ujumla utofauti upo lakini si wa kiwango kikubwa. Utofauti mwingi upo katika hatua fulani tu za ukuaji mfano katika umri wa miaka chini ya 15 watoto wa kiume wamekuwa na uwezo mkubwa kimahesabu ukilinganisha na wanawake wakati wakati wakike wanakuwa nauwezo mkubwa katika lugha na sanaa.

Katika umri mkubwa utofauti huu unakuwa mdogo zaidi kiasi ambacho hakishawishi kuleta utengano kijinsia katika utendaji.

Kuelekea  usawa wa kweli Wanawake wanahitaji Kubadilika Kwanza

Wanawake wenyewe ndio chachu ya mabadiliko ya kweli. Kuwa na nafasi sawa au nyingi zaidi katika utendaji na uongozi peke yake hakutafanya waheshimiwe zaidi wala kufuta mtazamo ule wakizamani hata sasa hivi ambao wanawake wanachukuliwa kama dhaifu na wasioweza. Bali kutupilia mbali nafasi za upendeleo,kujitokeza katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii na wanawake kwa wanaume kupewa nafasi sawa na kutumia vigezo sawa katika kuwateua na kuchagua ili kushika nafasi za uongozi,kazi na hata katika maendeleo ya masomo katika taasisi za elimu.

Vitu Ambavyo Vinaongeza Unyanyapaa waKijinsia kwa Wanawake:

Kuna mambo ambayo yanarudisha nyuma kufikiwa kwa lengo la usawa wa kijinsia na ni budi kuangaliwa kwa umakini na kubadirishwa

i.  Siku za Wanawake na  naVyama:

Dhana hii inaongeza utofauti,wanaume hawana vyama,hawalalamiki. Kulalamika kunaashiria udhaifu kwa namna nyingine. Kihistoria na kiutamaduni wale ambao wanajiona kuwa na hali ya chini tu ndio huanzisha harakati za aina hii na kifikra huwashusha zaidi kuliko kuwapandisha.

ii. Nafasi Maalumu katika Uongozi au Elimu:
Hizi zitolewe na wanawake wasikubali,washindane katika vigezo sawa na wakishinda wataheshimika zaidi  na kubezwa kwao kutakufa kifo cha asili.

iii: Wasichague kazi za kufanya:
Wanawake wanauwezo wa kufanya mambo mengi hata yote ambayo wanaume wanafanya,wasijishushe na kuwaachia mambo hasa magumu tu kuwa ya wanaume.

iv. Mila za Kulipia Mahali katika Kuolewa kwa Mwanamke:
Japo mila ni kitu muhimu lakini hii ni lazima iangaliwe kwa namna nyingine. Wanawake wasinunuliwe kwa mahali. Dhana ya kulipa mahali ni kununua,tubadilishe hili kuendana na wakati.

v. Kuwajibika katika Masuala ya Familia:
Wanawake watoe mchango sawa na wanaume katika kuendesha familia. Wanawake hata wakiwa na nafasi hawachangii sana mahitaji ya nyumbani na kuacha hilo kama jukumu la mwanaume.

 

Inakubalika kutokana na utafiti kuwa wanawake wana uwezo wa kufanya sawa na wanaume lakini mila na utamaduni wetu huenda unachangia kwa kiasi kikubwa kutofikia usawa wa kijinsia. Na harakati zetu hazitafikia lengo mpaka hatua zitakapochukuliwa na hasa na wanawake wenyewe.

Je kuna sehemu nyingine unahisi inadidimiza usawa wa kijinsia? Changia mada kwa kuandika katika kisandukucha hoja hapa chini.

 

 

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment