Fedha na Uchumi

Vitu muhimu kufanya gari lako liishi muda mrefu

Auto Checks

Magari ya kisasa yanatarajiwa kupita kilometa 300,000 ikiwa bado na hali nzuri kama itafanyiwa matengenezo ya mara kwa mara.

Baadhi ya matengenezo kikweli unaweza kuyafanya mwenyewe ,vinginevyo basi peleka katika gereji ya karibu.

Vifaa na nyezo:
Ili kufanya mwenyewe utahitaji kuwekeza kidogo katika vifaa na nyezo za kuanyia matengenezo. Utahitaji kujifunza kidoogo toka kwenye chuo cha karibu cha ufundi au toka kwa mafundi wa magari. Ikiwezekana itahitaji kulipa ada kidogo lakini itakusaidia kuokoa fedha nyingi siku za mbele.

Internet ni sehemu nyingine itakayokusaidia kujifunza juu ya magari, jaribu youtube .com na tafuta habari kuhusiana na matengenezo ya magari nautapata video zitakazo kusaidia kujifunza.

Kwanza itakubidi uandae daftari la kutunzia kumbukumbu za matengenezo ya gari lako.

Mara ya mwisho ulipobadili oili ,tairi au chujio la hewa (“Air Filter”)

Tunza kumbukumbu:
Pia utunza kumbukumbu za jinsi unavyotumia mafuta. Lita za mafuta ulizoweka na tarehe na uangaliae umbali uliotumia kabla ya mafuta kuisha. Taarifa hizi zitakusaidia kuona kama gari lako linahitilafu au la.
Kitabu cha mwongozo wa mmiliki wa gari (Owner’s manual) yako kitakupa maelezo muhimu juu ya matengenezo ya gari lako kulingana na umbali gari lako limetembea.

 

Matengenezo katika kilometa 3000
Inafahamika kwa wengi kuwa ni muhimu kubadili mafuta katika injini yako kila baada ya gari kutembea kilomita 3,000.

Hilo ni muhimu sana, katika umbali huu matengenezo ni muhimu kama unataka gari lako liishi maisha marefu likiwa na hali nzuri.

Inashauriwa vitu vifuatavyo viangaliwe na kubadilishwa

  1. Filta za mafuta na hewa

Kuangalia kama ni chafu au zimeziba, filta chafu husababisha utumiaji wa mafuta zaidi

  1. Matairi

Kuangalia kama matairi yameisha au yamenyooka. Pia kama nati zimefungwa vizuri

  1. Mipira ya kupitisha mafuta na gesi

Kuangalia kama mipira imeziba au kutoboka na kama inavujisha mafuta au gesi

  1. Betri na nyaya zake

Maji katika betri yanatakiwa kuangaliwa na ikiwezekana kubadilishwa,pia kuondoa kutu katika nyaya za betri. Hii inaweza kuondolewa na brashi ya waya au msasa.

 

Katika kilometa 5000-10,000
Rekebisha mzunguko wa matairi yako (Wheel Balancing) kila baada ya kwenda kilometa 5000-10,000. Hii husaidia matairi kuisha kwa uwano sawa pande zote za tairi na hivyo kuyatumia kwa muda mrefu zaidi.

Matairiyaliyo mazima zaidi yanatakiwa yawekwe mbele

Angalia upepo wa tairi mara kwa mara na angalia kama tairi zinaisha upande mmoja.

 

Katika kilometa 15,000:
Badili filtaya hewa kila baada ya km 15,000. Hewa safi Filta safi ya hewa inaboresha matumizi mazuri ya mafuta na kukusaidia kupunguza gharama.

Filta ya Hewa chafu inaweza kusababisha injini ya kushindwa kuenda vizuri (“Miss”)

Kwa wakati huu unapaswa pia kuangalia breki ,angalia viatu na padi za breki kama ziko sawa.

Mafuta ya breki pia yaangaliwe kama yako katikakiwango kinachofaa.

Jaribu breki na sikiliza kama kuna kelele au usukani una tingishika,hii inaweza ikawa dalili kuwa breki zinahitaji kubadilishwa.

 

Katika Kilometa 30,000
Angalia transmission fluid. Kitabu cha umiliki wa gari kinaeleza aina ya mafuta yanayotakiwa kutumika na kwa kiwango kipi.

Wakati huu utatakiwakubadili plagi za kuwasha engini.

Katika Kilometer 50,000

Mabadiliko ya koolanti yanatakiwa kufanyika.

Aina na viwango vya koolanti vimeelezwa katika kitabu cha umiliki wa gari. Hakikisha aina ya koolant tajwa ndiyo zinazotumika na si vinginevyo.

Kumbuka kutunza gari lako vyema. Unatakiwa kupaka rangi pale inapofaa kulifanya gari liwe katikamwonekano mzuri kwa muda mrefu.

Safisha gari mara kwa mara,hii itasaidia pia kupunguza chumvi mabayo hula chuma ya bodi ya gari. Pia weka nta (wax) baada ya kuosha itasaidia kupunguza madhara ya jua na kutunza rangi ya gari lako. Hakikisha taa za gari zinafanya kazi. Badilisha glopu zilizoungu.

Kwa kufanya haya utalifanya gari lako liishi muda mrefu na libaki katika mwonekano mzuri.

Nakutakieni utunzaji mzuri wa magari y

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment