Michezo

Wachezaji 10 Vijana Mahiri katika Kombe la Dunia 2014

Kuna wachezaji mahiri na maarufu duniani ambao wanashiriki katika kombe la dunia 2014 Brazil,lakini kuna wale ambao ni wachanga lakini wenye vipaji vikubwa ambao wataleta mvuto mkubwa katika mashindano haya.

Hapa tunawataja wachezaji 10 vijana ambao wanaumri mdogo usiozidi miaka 22.

 

Christian Atsu
Timu: Ghana
Umri: 22

Christian-Atsu1

Winga mwenye kasi na ustadi wa hali ya juu.

Amewahi kuchezea Porto ya Ureno na hatimaye kuhamia Chelsea ambayo imemuuza kwa mkopo katika timu ya Vitesse ambako amekuwa akufanya vizuri sana.

Anategemewa kutoa msaada mkubwa sana kwa timu yake ya Ghana wakiwa wanagombana katika kundi lao (Kundi D) gumu kabisa dhidi ya  Ujerumani,Ureno na Marekani.

 

Ross Barkley
Timu: Uingereza
Umri: 20


Kuna idadi ya nzuri vijana toka timu ya Uingereza ambao wana uwezo wa kuwa katika nafasi za juu katika mashindano ya mwaka huu.

Wakiwemo Alex Oxlade-Chamberlain na Raheem Sterling.

Hata hivyo, Ross Barkley wa Everton anapata kura nyingi zaidi.

Umahiri wake katika ligi ya Uingereza mwaka huu imemweka Barkley katika nafasi za juu kabisa katika kiwango cha soka kwa wachezaji vijana.

Hivyo ni matehgemeo atang’ara Brazil mwaka huu na kutia mvuto.

 

Mario Gotze
Timu: Ujerumani
Umri: 21

Mario-Gotze
Ukiangalia toka alipoanza kucheza na mafanikio aliyoyapata ni ngumu kuamini kuwa Gotze ana umri wa miaka 21 tu.

Kiungo huyu wa kati amenyakua ubingwa wa Bundesliga mara tatu na timu yake ya Beyern Munich na ameshiriki katika mashindano ya Mabingwa wa Ulaya mara kadhaa.

Ana kipaji na ni mbunifu akiwa uwanjani pia ni mtaalamu katika kufumania nyavu za timu pinzani.

Bilashaka atakuwa mojawapo ya wachezaji wa kuvutia katika Kombe la Dunia 2014-Brazil mwaka huu.

 

Romelu Lukaku
Timu: Ubelgiji
Umri: 21
lukaku
Amecheza kwa mkopo Everton toka West Bromovich katika ligi ya Uingereza 2013/2014 na kuonyesha kiwango kikubwa sana.

Ni mshambuliaji hatari ambaye eamekuwa akiwasumbua sana mabeki uwanjani.

Aliifungia timu yake magoli 12 katika mechi 24 alizocheza katika ligi ya Uingereza msimu uliopita.

Ni mchezaji anayetegemewa kuonyesha cheche zake katika mashindano haya pia.

 

 

Neymar
Timu: Brazil
Umri: 22
Neymar
Mchezaji mwingine hatari ,mwenye kasi na uchu wa magoli ni Neymar. Tayari amesha funga magoli mawili kwa timu yake katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Croaria tarehe 12 June 2014.

Ni mchezaji aliyepata mafanikio makubwa katika soka nchini kwake akichezea Santos na kimataifa hasa baada ya kwenda Barcelona ya Uhispania.

Tegemea makubwa toka kwa kijana huyu katika mashindano haya nyumbani kwao Brazil.

 

Kenneth Omeruo
Timu: Nigeria
Umri: 20
Kenneth-Omeruo
Anacheza kwa mkopo Middlesbrough kutoka Chelsea. Omeruo ni mchezaji mzuri mwenye kasi. Amechezea timu yake ya taifa mara 17 na mara zote ametoa mchango mkubwa.

Ni mchezaji ambaye ana uwezo mkubwa wa kujihami na anategemewa sana kuzizuia timu pinzani katika kundi lao la F wakicheza dhidi ya Argentina na Bosnia & Herzegovina katika hatua ya makundi.

 

Paul Pogba
Timu: Ufaransa
Umri: 21
Paul-Pogba
Pogba alianza kuonekana baaada ya kuhama toka Manchester United kwenda Juventus mwaka 2012.

Sasa hivi ni mojawapo ya wachezaji wa kati maarufu Ulaya.

Ni mgawaji mazuri wa mipira yenye kuleta magoli na hivyo anawekwa katika kundi la wachezaji hodari mwaka huu.

 

Juan Fernando Quintero
Timu: Colombia
Umri: 21
Juan-Fernando
Hivi sasa anachezea Porto ya Ureno. Umahiri wake umepelekea kufananishwa na Lionel Messi kutokana na ujuzi wake katika kutumia mguu wa kushoto na kushambulia na anaweza kucheza katika nafasi kadhaa.

 

Diego Reyes
Timu: Mexico
Umri: 21
Diego-Reyes
Ni mlinzi mlinzi mahiri,alihamia Porto mwaka 2013 toka America akichezea ligi ya Mexico.

Pamoja na ukweli kwamba amekuwa akicheza Timu ya pili ya Porto , Reyes ni mchezaji mzuri na mwenye mategemeo ya mafanikio makubwa siku za mbele.

Ni mojawapo ya wachezaji wanaotegemewa katika timu yake mwaka huu na huenda akawashagaza wengi.

 

Raphael Varane
Timu: Ufaransa
Umri: 21
Raphael-Varane
Anafikiriwa kuwa mojawapo ya mabeki bora barani Ulaya.

Varane alijiunga na Real Madrid akiwa na umri wa miaka 18 tu mwaka 2011, na tayari amecheza zaidi ya mechi 60 katika timu yake ya Los Blancos na haraka amekuwa moja ya mabeki wakutumainiwa sana.

Akiwemo uwanjani ni vigumu sana kwa wapinzani kumpita.

 

Kuna wengine wengi ambao hawajatajwa, hebu waongezee basi katika boksi la maoni hapo chini.

 

Andika katika “Comment” na kisha bonyeza “Post Comment”

 

 

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment