Michezo

Wachezaji Bora wa Mpira wa Miguu wa Wakati Wote: Wachezaji 10 Bora

PELE

Vipaji vipya vya mpira wa miguu vimekuwa vikiibuka kila siku na kuacha historia kubwa duniani.

Lakini kuna wachezaji ambao wanatajwa kuacha historia kubwa katika kusakata kandanda duniani kiasi ambacho si rahisi kusahaulika katika historia,hawa ni wachezaji bora wa mpira wa miguu wa wakati wote.

Wachezaji hawa wameweka historia katika ulimwengu wa soka kutokana na juhudi zao binafsi na vipaji vikubwa walivyojaliwa katika mchezo huu na kuwawezesha kujipatia umaarufu mkubwa na wapenzi lukuki duniani kote.

Ningependa kutaja majina ya wachezaji bora wa mpira wa miguu 10 ambao watakumbukwa siku zote katika soka, vigezo vilivyotumika ni kuwa na wapenzi wengi,kucheza kwa muda mrefu na kupata tuzo kubwa katika soka duniani.

 Nafasi ya 10: Eusébio (1958-1978)-Ureno

Eusébio

Kwa kizungu aliitwa “The Black Panther” yaani “Paka Pori Mweusi” toka Ureno. Alizaliwa Msumbiji na kucheza soka Ureno.

Kabla ya Ronaldo alitambulika kuwa ni mchezaji bora kuwahi kutokea nchini Ureno.

Nafasi ya 9: Zinedine Zidane -Ufaransa

zidane

Alifunga mabao yote mawili katika mechi ya fainali ya kombe la dunia mwaka 1998 na kuifanya Ufaransa kuwa mabingwa wa dunia.

Aliisaidia timu yake ya Ufaransa katika kombe la dunia la mwaka 2006 japo hawakufanmya vizuri sana.

Alifunga magoli lukuki akiwa Real Madrid an kuisaidia timu yake kufanya vizuri katika ligi na ubingwa wa ulaya.

Nafasi ya 8: Cristiano Ronaldo -Ureno

ronaldo

Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao. Mwaka 2014 alitimiza mabao 400 akiwa na umri wa miaka 28 tu. Ana uwezo wa kumiliki mpira stamina na anajua goli lilipo.

Nafasi ya 7: Ferenc Puskás (1944-1966) -Hungari

Ferenc Puskás

Mojawapo ya wafungaji bora wa magoli. Alikuwa na wastani wa angalau goli moja kila mechi aliyocheza.

Alikuwa mchezaji wa timu ya taifa Hungari na klabu ya Real Madrid. Alifunga magoli 7 katika fainali mbili za ubigwa wa ulaya.

Nafasi ya 6:  Alfredo Di Stéfano (1943-1966) – Argentina/Hispania

Alfredo Di Stéfano

Alifunga mabao katika mashindano ya ulaya mara tano mfululizo. Alichezea klabu ya Real Madrid katika miaka ya 50 na kuwika sana.

Nafasi ya 5:  Franz Beckenbauer (1964-1984)-Ujerumani

Franz Beckenbauer

Alichezea klabu ya Bayern Munich ambako alishida Bundesliga mara tano na kombe la ulaya mara tatu.

Alikuwa na uwezo wa kucheza beki na kushambulia.

Nafasi ya 4: Johan Cruyff (1964-1984)-Uholanzi

Johan Cruyff

Mdachi aliyechezea Ajax na Barcelona katika miaka ya 60 na 70. Alijulikana kama mchezaji bora wa ulaya wakati huo. Maarufu kwa kucheza mfumo wa “Total Football” ambabo wachezaji wanabadirishana nafasi wakati wa kupeana basi na kuwafanya wachezaji wote wa timu kushiriki.

Alipata tuzo 3 za mchezaji bora wa ulaya na kushinda vikombe 8 na Ajax

Nafasi ya 3: Lionel Messi -Argentina

messi

Japo ni mchezaji wa siku hizi za karibuni tu lakini Messi ni mchezaji aliyeonesha kiwango cha hali ya juu kabisa na anaendelea kufanya hivyo. Amepata tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara tatu na mchezaji bora wa kombe la dunia mwaka 2014 (japo wengi waliona kuwa hakustahili)

Ameisaidi sana timu yake ya Barcelona kupata mafanikio katika kipindi alichoichezea na bado anaendelea kufanya hivyo.

Alivunja rekodi ya Gerd Muller ya kufunga mabao 91 katika msimu mmoja mwaka 2012

Messi ni mchezaji pekee aliyewahi kuwa mfungaji bora katika Ligi ya Washindi Ulaya mara 4 mfululizo

Mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia (FIFA/Ballons d’Or ) mara nne mfululizo

Mchezaji kijana kufunga mabao 200 katika ligi ya Hispania-La liga.

Mfungaji bora wa wakati wote wa Bacrcelona katika mechi rasmi za klabu ya Barcelona.

Mchezaji mkongwe na hatari Maradona anamtaja Messi kuwa juu na pengine kumzidi.

Nidhamu yake ya hali ya juu katika soka inamfanya awe juu ya wengine.

 Nafasi ya 2: Maradona (1976-1997) -Argentina

Argentina Diego Maradona, 1986 World Cup

Ni mojawapo ya wachezaji walikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza na kuudhibiti mbira uwanjani. Alifunga goli la ushidi katika fainali ya kombe la dunia mwaka 1986 dhidi ya Uiengereza goli lililozua utata na kuitwa “Goli la mkono wa Mungu” ikisemwa kuwa Maradona alifunga kwa mkono.

Hakuwa na nidhamu sana uwanjani na hata nje ya uwanja lakini uwezo wake mkubwa wa mchezo unafahamika na atabaki katika kumbukumbu

 Nafasi ya 1: Pele (1956-1977) – Brazili

pele1

Jina kamili ni Edson Arantes do Nascimento. Anashika namba moja katika orodha ya wachezaji bora wa mpira wa miguu duniani kuwahi kutokesa

Alishinda Kombe la dunia mwaka 1958, 1962 na 1970 ni mchezaji pekee aliyewahi kushinda kombe ladunia mara tatu.

Alikuwa mchezaji mwenye akili na kasi ya ajabu. Alikuwa anauwezo mkubwa wa kukimbia na mpira nakufunga mabao. Alifunga mabao 1,000 katika kipindi chake cha kucheza mpira.

Pele asemwa kuwa mchezaji toka dunia nyingine kutokana na kuwaacha wengine mbali sana kwa kiwango.

 

Video za Pele Uwanjani

 

Wengine..

Kuna wengine wengi wazuri na orodha ni fupi sana kuweza kuwaweka. Wachezaji kama Zico,Garincha, Lonald Lima, George Best na wengine wengi.

Tupe majina ambayo unafikiri yanatakiwa kuwepo katika 10 bora ya wachezaji bora wa mpira wa miguu wa wakati wote kwa kuandika katika kisanduku hapo chini.

Asanteni

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment

1 Comment