Biashara na Ujasiriamali Fedha na Uchumi Mafanikio Mitindo ya Maisha

Kwanini Wageni Wanafanikiwa Zaidi Kuliko Wenyeji?

Wageni Wanafanikiwa Zaidi Kuliko WenyejiUkifuatilia utagundua katika nchi yoyote duniani,watu wanaokuja toka nchi nyingine au eneo jingine kwa minajili hasa ya biashara wanafanikiwa zaidi kuliko wenyeji wa nchi au eneo hilo.

Nini sababu? Hebu tufuatilie pamoja katika makala hii ambapo nitakupa sababu za msingi zinazowafanya wageni kufanikiwa zaidi kuliko wenyeji wa eneo husika.

Pia soma: Hatua 10 za Kuanzisha Biashara Yenye Mafanikio

Sababu 5 Kubwa zinazowafanya Wageni Kufanikiwa Zaidi Kuliko Wenyeji:

  1. Kuwa na lengo Moja:

Wahamiaji au wageni wanafanikiwa kubaki na lengo lao kuu na hivyo kufanikiwa kuweka nguvu na msukumo katika lengo kuu ambalo ni kutafuta maisha bora zaidi au kukuza mitaji na biashara zao.

  1. Kuwa Mbali na Ndugu na Jamaa Masikini

Ndugu,jamaa na marafiki wanaweza kukupandisha lakini pia kukushusha katika maendeleo yako. Kwahiyo aina gani ya watu unahusiana na kuwa nao karibu wanachangia sana safari yako ya mafanikio au kuanguka kwako. Fanya utafiti kuona una watu wa aina gani wanaokuzunguka na chagua kubaki na wale wenye kukupandisha juu na wenye mawazo chanya.

Ukiwa na watu masikini au wenye mawazo hasi ya kimasikini basi utabaki kuwa kama wao.

Ukiwa mgeni kwenye nchi au eneo fulani unanafasi kubwa ya kuwaepuka ndugu na jamaa na marafiki hasi wenye kukuvuta nyuma. Hii ni sbabu nyingine  inayowafanya wageni kufanikiwa zaidi. Hawana ndufu,marafiki na jamaa wengi wanaowavuta kurudi nyuma.

Ukiwa karibu na nyumbani kwenu ambako familia ni kubwa na mahitaji ni makubwa, ni ngumu sana kujikwamua na kwenda mbele sababu kila jicho lenye mahitaji litakuangalia. Ukiwa mbali inapunguza tatizo hilo na mategemeo toka kwa ndugu na jamaa wenye mahitaji na wanaokutegemea uwasaidie yanakuwa chini.

  1. Wageni Unajiweka Kwenye Kundi Maalumu

Wageni wanajiweka au wanawekwa na wenyeji katika kundi maalumu,kundi la juu. Hivyo wanatakiwa kuishi katika nafasi hiyo. Wanategemewa wataishi nyumba bora na kufanya kazi nzuri. Ili kubakisa hadhi hiyo ya juu wanatakiwa kujituma zaidi kuliko wale wenye hadhi ya chini.

Ukiwa karibu na kwenu unajilinganisha na wale wanaokuzunguka na kama watakuwa na hali za chini basi na wewe utabaki hapo.

  1. Wageni Wanasaidiana Baina Yao

Ni rahisi kwa mgeni kumsaidia mgeni mwenzake kuliko mwenyeji kwa mwenyeji au mwenyeji kwa mgeni. Hasa kama wanatoka sehemu moja au nchi moja.

Hata ndani ya nchi utaona watu wanaotokea katika mkoa au mji mmmoja wanasaidiana zaidi katika kupandisha hali zao za maisha. Angalia mfano wa makabila ya Wachaga na Wahaya nchini Tanzania. Kila penye fursa na kuna mtu wa kabila lake atampa kipaumbele yeye kwanza.

  1. Ni Rahisi Kuona Fursa Ugenini

Ukifanya utafiti mfupi utaona hata wewe mwenyewe unakawaida ya kuona fursa nzuri zaidi unaposafiri,ukiwa njiani au ukiwa umefika uendako(ugenini). Akili inafunguka kwasababu ya kuona vitu tofauti na vile ilivyovizoea. Halii hii ya akili kuwa makini na vitu vipya inawasaidia wageni kuona fursa za mafanikio kuliko wenyeji wa eneo hilo. Mfano wakati dunia nzima inatamani kuja Tanzania kuona na kupanda mlima Kilimanjaro,sisi wenyewe (Watanzania) hatuna hata mpango wa kufanya hilo na hatuoni umuhimu wala muto wowote.

Mwisho:

Kama tilivyoona, ni rahisi kwa wageni kufanikiwa nje ya eneo lao walilokulia au kuishi kwa muda mrefu. Mifano iko ya kutosha nchini na hata katika mji unaoishi hata kijijini kwako. Wale wanaohamia wanafnikiwa zaidi kimaisha.

Kwa hiyo ule usemi wa “naenda mjini kutafuta maisha” huenda ukawa na ukweli fulani, wale wanaotoka kwenda mbali na kwao wana nafasi kubwa ya kufanikiwa kuliko wakibaki makwao.

Hata kama hutaenda na kubaki huko moja kwamoja ,hata kusafiri tu na kurudi kwenu kutasaidia kufanya maendeleo zaidi kwa kuwa utakuwa umefungua macho kwa kuona wengine wanachofanya huko nje.

Ni matumaini yangu kuwa makala hii imekuongezea kitu katika juhudi zako za kuboresha maisha yako. Kama ndivyo basi washirikishe na wengine kwa kubofya vitufe vya mitandao ya kijamii chini ya makala hii. Kama una maoni tafadhali tuandikie kwenye kisanduku cha maoni hapa chini.

Facebook Comments

Facebook comments

Leave a Comment